Mabondia wanne wa Tanzania wamewasili Urusi kupambana akiwemo Dullah Mbabe

Mabondia wanne wa Tanzania wamewasili Urusi kupambana akiwemo Dullah Mbabe

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mabondia wanne wa Tanzania akiwemo Dullah Mbabe wamewasili nchi Urusi kuzichapa na mabondia wa Urusi ambao awali Dullah Mbabe aliwataja kuwa wanapiga sana, lakini ameamua kwenda.

Dullah Mbabe atapambana na Pavel Silyagin kuwania ubingwa wa Asian Pacific mkanda wa WBO. Twaha Kiduku atapambana na Bek Nurmaganbet ambaye aliwahi kupiga Dullah Mbabe.

Nasibu Ramadhani atapambana na Yergniy Pavlov pia Alphonce Mchumiatumbo atapambana na Vartan Arutyunyan.

Wanapigana leo, Mei 20, 2021
 
Twaha kiduku alimpunguza majigambo ajitahidi huko urusi asituangushe
 
Hii Team sijui kama kuna mtu atatoboa asia sio kuzuri kwa afya
 
Huyu jamaa ameshawakatisha tamaa 😂😂😂
 
Jamaa si alikataa kupambana na warusi? Imekuaje tena?
 
Back
Top Bottom