Omary 1998
New Member
- Jun 20, 2024
- 3
- 3
Serikali ya Tanzania kupitia mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) wamekuwa wakitoa ripoti kunako mahesabu ya mwaka katika nyanja mbali mbali na kufanikiwa kubaini makamilifu katika sekta mbali mbali Hali kadhalika na madhaifu katika sekta mbali mbali hapa nchini kunako mahesabu ya fedha za uma. Hovyo basi ripoti hii ya CAG imekuwa ikifungua mwanga mkubwa kw raia wa Tanzania kunako kutambua utendaji sahihi wa mamlaka mbali mbali hapa nchini .
NINI MADHAIFU YANAYOBAINIKA KUTOKANA NA RIPOTI YA CAG ?
Miongoni mwa madhaifu ambayo Kila mwaka yamekuwa yakiripotiwa na CAG ni upotevu wa mabilioni ya pesa za uma Hali inayopelekea kuleta sitofahamu katika taifa letu na ikifahamika wazi kuwa upotevu wa mabilioni hayo hufanywa na watu walioko madarakani katika sekta zao.
Kila mwaka watanzania wamekuwa wakishudia jopo kubwa Sana la wizara mbali mbali na taasisi za uma zikishukiwa juu ya upotevu wa pesa za nchi ambapo serikali imekua ikikemea Sana Hali hiyo ila Bado ubadhilifu umekuwa ukijirudia katika mamlaka mbali mbali hapa nchini Hali inayopelekea kuchangia kudolola Kwa maendeleo ya taifa letu kutokana na kundi la viongozi wachache kutumia pesa za nchi Kwa kujinufaisha wao binafsi.
KWANINI KILA MWAKA UBADHILIFU UMEKUWA UKIJIRUDIA KATIKA RIPOTI YA CAG ?.
Kila mwaka mamlaka mbali mbali zimekuwa zikibainika kufanya ubadhilifu wa mabilioni ya pesa za nchi kutokana na sababu zifuatazo;
(a). Serikali kushindwa kupambana Kwa ufanisi juu ya wabadhilifu wa pesa hizo Hali inayopelekea mamlaka hizo kuchukulia ni kama Hali ya mazoea na hatimae badala ya kupungua Kwa ubadhilifu Bali Hali inazidi kuwa mbaya mwaka Hadi mwaka na mbaya zaidi baadhi za mamlaka zimekuwa zikituhumiwa mara Kwa mara pabila kuona mabadiliko yoyote chanya katika mamlaka hizo.
(b). Serikali kushindwa kuandaa mpango kazi endelevu ambao utakua chachu juu ya washukiwa wa ripoti hiyo ya CAG. Hali inayopelekea serikali kutoweza kupambana ipasavyo juu ya tatizo Hili na hatimae kupelekea kupuuzwa Kwa shutuma hizi .
KWANINI WASHUKIWA WA RIPOTI YA CAG HAWACHUKILIWI HATUA MADHUBUTI?.
Kwa upande wangu naona kua sababu inayochangia washukiwa wa ripoti ya CAG kushindwa kushughulikiwa ipasavyo ni kutokana na mamlaka ambazo zimekuwa zikipewa jukumu la kufuatilia washukiwa hao ambapo changamoto kubwa utakuta miongoni mwa wanaopewa jukumu Hilo nao ni miongoni mwa washukiwa Hali inayopelekea shutuma hizo kutekelezwa pa bila kushughulikiwa ipasavyo. Hali hii imepelekea kuchangia raia kutokuwa na Imani na serikali Hali inayopelekea kudolola Kwa maendeleo katika sekta mbali mbali nchini.
JE SERIKALI IFANYE MABORESHO GANI KUTOKANA NA RIPOTI YA CAG ?.
Kwa upande wangu nashauri serikali iunde jopo maalumu la wanasheria ambalo litakua sambamba na CAG katika utendaji wake wa kazi. Jopo Hili linaweza kua kuanzia ngazi ya taifa Hadi wilaya ili kuongeza ufanisi zaidi wa utandaji kazi ili kuweza kuleta matokeo chanya katika taifa letu.
Baada ya kuundwa Kwa jopo Hili likabidhiwe Kwa CAG ambapo atakuwa akishirikiana nalo juu ya uwajibikaji wake.
Pia nashauri serikali inaweza anzisha mahakama maalumu itakayokuwa na jukumu Moja tu la kushughulikia makosa ya ubadhilifu wa fedha za uma lengo na madhumuni ikiwa ni kuongeza ufanisi wa ufatiliaji na utoaji hukumu juu ya makosa ya uhujumu uchumi nchini Tanzania. Mahakama hii inaweza jengwa Kwa Kila Kanda mahakama Moja ambayo itakuwa ikishughulikia makosa ya ubadhilifu katika Kanda husika .
NINI MAJUKUMU YA JOPO HILI ?.
Jopo Hili la wanasheria Kwa kushirikiana na CAG litakua na majukumu yafuatayo;
(a). Kila baada ya kusomwa ripoti ya CAG jopo Hili kazi yake itakua ni Moja tu kuwafungulia mashtaka washukiwa wote waliosomwa katika ripoti hiyo .
(b). Kabla ya kuisha mwaka jopo Hili likishirikiana na CAG wawe wanasoma ripoti nyingine inayohusu hatima ya washukiwa waliosomwa katika ripoti ya mahesabu ya serikali ili kuwaeleza watanzania ni hatua zipi zimechukuliwa juu ya Kila muhusika wa ubadhilifu wa pesa za nchi.
Hivyo basi Kwa kua CAG ndie anaekuwa amebaini wabadhilifu basi na jukumu la kushughulikiwa Kwa wabadhilifu hao liwe chini yake ili kuchochea ufanisi wa jambo Hilo ambalo naimani litaleta matokeo chanya katika taifa letu la Tanzania.
NINI FAIDA ZA MABORESHO HAYA ?.
Kwa mtazamo wangu naona wazi kabisa kama mabadiliko haya yatafanyika basi yataleta mabadiliko Sana kutokana na ripoti ya CAG kama ifuatavyo;
(a). Ikiwa jukumu la kuwachukulia hatua wabadhilifu wa pesa za uma litakua likiratibiwa na CAG mwenyewe hakika litakua ni lenye kuleta matokeo haraka zaidi na Kwa ufanisi wa Hali ya juu zaidi kuliko ilivyokuwa awali ambapo CAG alikuja akikabidhi wabadhilifu Kwa mamlaka zingine.
(b). Pia maboresho haya yatachochea usimamizi na udhibiti mkubwa Sana wa pesa za uma unaofanywa na mamlaka mbali mbali hapa nchini.
(c). Halikadhalika maboresho haya yatachangia nidham kubwa Sana ya utendaji wa viongozi mbali mbali katika mamlaka mbali mbali mana naimani wengi watakuwa ni wenye kuchukuwa hatua stahiki na Kwa wakati maalumu ambapo naimani itakua ni kama funzo Kwa wengine.
( d). Pia maboresho haya yatachochea utumiaji sahihi wa fedha za uma kama zilivyopangwa Hali itakayochochea maendeleo chanya katika taifa letu katika kizazi hichi na kizazi kijacho.
Hivyo basi serikali inapaswa kuweza kufanya maboresho hayo ili kuweza kuongeza ufanisi kunako utandaji kazi wa CAG ili kuweza kuleta matokeo chanya juu ya ripot yake. Naimani kama maboresho haya yatafanyika Kwa weledi kutachochea wananchi kua na Imani zaidi juu ya serikali Yao na pia maboresho haya yatachochea maendeleo ya kiuchumi katika taifa letu na hatimae kupiga hatua kutoka sehemu Moja Hadi nyingine.

Upvote
5