Elipa malipo
Member
- May 27, 2024
- 7
- 4
Mnamo tarehe 9 Desemba 1961, Tanganyika ilijipatia uhuru wake kutoka kwa koloni la Kiingereza. Wakati huo, alikuwepo gavana aitwaye Sir Richard Turnbull. Gavana wa kikoloni huku Tanganyika alikuwa ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ambaye pia anajulikana kama baba wa taifa. Tanganyika ilikua nchi huru baada ya kujinasua kutoka kwa mikono ya wakoloni, na ilikuwa taifa lenye makabila mbalimbali yaliyokuwa na ukabila kama Wakurya, Waha, Wanyamwezi, na Wakara. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliunganisha taifa kwa kutumia lugha moja ya Kiswahili. Mnamo tarehe 26 Aprili 1964, Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kutengeneza taifa la Tanzania. Muungano huu uliweza kuondoa ubaguzi (umimi na usisite).
Mwaka 1977, Tanzania iliunda chama cha siasa ambacho kiliundwa kutokana na TANU, na chama hicho kilijulikana kama CCM. Ndicho chama tawala mpaka leo. Tangu uhuru, tumekuwa na awamu mbalimbali za viongozi ambapo awamu ya kwanza iliongozwa na baba wa taifa, awamu ya pili na Ali Hassan Mwinyi, awamu ya tatu na Benjamin Mkapa, awamu ya nne na Jakaya Mrisho Kikwete, awamu ya tano na Dr. John Pombe Joseph Magufuli, na awamu ya sita inaongozwa na Mama Samia Suluhu Hassan. Wote hao ni waheshimiwa marais wa awamu tofauti nchini, na kila mmoja kwa kiasi chake ameleta mabadiliko makubwa nchini. Mpaka sasa, Tanzania ni nchi yenye uchumi wa kati, yenye wakazi milioni sitini na moja, kati yao wanawake ni takribani milioni thelathini na moja huku wanaume wakiwa takribani milioni thelathini. Tanzania ina takribani mikoa thelathini na tano na pia ina vyanzo mbalimbali vya maji kama mabwawa, maziwa na mito. Mfano wa maziwa ni Ziwa Tanganyika, Ziwa Nyasa, na Ziwa Victoria.
Tanzania pia ina madini kama dhahabu, almasi, tanzanite, na shaba. Pia kuna vyanzo mbalimbali vya nishati kama nishati ya maji inayozalishwa katika mabwawa kama Mtera, Nyumba ya Mungu, Kidatu, na Bwawa kubwa la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Vyanzo hivi vinaweza kusaidia nchi yetu kwa kiasi kikubwa na kushusha gharama za maisha, hususan gharama za nishati ya umeme. Tanzania ina hifadhi mbalimbali za wanyama kama Hifadhi ya Serengeti na zile za akiba kama Lubondo, Tarangire, Manyara, na Mikumi. Hifadhi hizi zinasaidia katika pato la taifa na kupanua wigo wa ajira. Sekta ya utalii na mali asili inapaswa kuboreshwa ili kuendana na soko la kimataifa. Tanzania ndio nchi pekee barani Afrika iliyo na mlima mrefu na ambao ni wa tatu kwa urefu duniani. Taifa la Tanzania linazalisha mazao mbalimbali kama kahawa kutoka mkoani Kagera, alizeti kutoka mkoani Singida, pamba kutoka mikoa ya Morogoro, Mwanza, na Shinyanga, na mahindi yanayozalishwa katika mikoa yote.
Ili taifa liwe na maendeleo, linahitaji sera au siasa nzuri zinazojenga. Msingi wa kitu chochote huanzia chini, na ni dhahiri kuwa hakuna msingi unaoanzia juu. Viongozi wetu wa serikali wakawa na fikra zinazojenga, kwa sababu sera au mawazo ndio msingi wenyewe wa kuwa na taifa lenye maendeleo bora. Maendeleo yamegawanyika katika nyanja kuu tatu: kifikra, kisiasa au kimawazo, kijamii, na kiuchumi. Viongozi wakiweka mawazo yao katika matendo, ndipo maendeleo yanaonekana kwa nje. Maandiko matakatifu yanasema jinsi mtu aonavyo nafsi yake ndivyo alivyo. Kwa mfano, mtu akiwaza kuwa anaweza kusoma na kufaulu, hayo ni mawazo au fikra nzuri na fikra hizo zitampelekea kusoma na kufaulu. Akishafaulu, akajiliwa au akajiajiri, ataanza kupata kipato au ujira.
Tanzania inaweza kuwa na maendeleo zaidi kwa kuhakikisha kuwa ina viwanda vya kutosha vya chini, vya kati, na vya juu. Serikali inatakiwa kuhimiza wananchi wafanye kazi kwa bidii, walipe kodi, na kutumia bidhaa zinazozalishwa nchini zaidi ya zile zinazotolewa nje ya nchi. Pia, watu wahimizwe kujua lugha yao ya taifa kuliko ile ya kigeni ya Kiingereza. Nchi yoyote iliyo kwenye uchumi wa chini ina hali fulani ya utumwa, hivyo hatuna budi kujinasua kutoka kwenye huo utumwa. Watanzania tuna uwezo mkubwa wa kuwa na uchumi mkubwa barani Afrika na duniani kwa ujumla. Sekta zote zinapaswa kuchukua jukumu la kufanya kazi kwa pamoja kwani hakuna sekta ambayo inaweza kufanya kazi peke yake na tukawa na maendeleo.
Sekta kama ya afya inahitaji wataalam wa afya kutoka sekta ya elimu, na sekta ya elimu inahitaji sekta ya afya ili kutoa huduma kwa watumishi na viongozi. Sekta nyingine ni sekta ya ulinzi, maji na umwagiliaji, mipango na fedha, ofisi ya rais, tawala za mikoa na serikali za mitaa, uvuvi, kilimo na ufugaji, nishati, na madini. Serikali kwa ujumla inatakiwa kuhimiza wananchi wafanye kazi kwa bidii, walipe kodi, na kutumia bidhaa zinazozalishwa nchini. Pia, watu wahimizwe kujua lugha yao ya taifa kuliko ile ya kigeni ya Kiingereza ili kujinasua kutoka kwenye hali ya utumwa wa kiuchumi.

Upvote
2