SoC04 Maboresho Sekta ya Elimu Tanzania kwa miaka kumi na tano (15) ijayo

SoC04 Maboresho Sekta ya Elimu Tanzania kwa miaka kumi na tano (15) ijayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

cbs elite

New Member
Joined
Jun 29, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Maendeleo ni Jambo linalohitaji Jitihada kubwa na jumuishi katika Sekta Muhimu kama vile ELIMU, UTALII, VIWANDA, AFYA, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Kwa Uhakika Suala la maendeleo ni mchakato wa muda mrefu unaohitaji mikakati na akili kubwa katika kujipanga na kuutekeleza ili kuyafikia matunda yake kwa asilimia kubwa.
Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika inayopambania sana Maendeleo yake kwa maslahi ya Wananchi wake, hivyo kwa kuzingatia Kuwa ELIMU ni sekta yenye uhusiano mkubwa na Sekta zote yafuatayo ni maono yangu katika Kuboresha na kuhakikisha Maendeleo katika sekta ya ELIMU kwa muda wa miaka 15 ijayo;

1. KUANZISHA MFUMO MAALUMU WA USAFIRI KWA WANAFUNZI
Kwa Kiasi kikubwa Suala la usumbufu wakati wa usafiri kwa wanafunzi limekuwa likichochea kushuka kwa Ufaulu wa wanafunzi hasa kutokana na Kuchelewa kufika mashuleni vipindi vya asubuhi, kutumia muda mwingi njiani na pia kuchelewa kurudi majumbani. Hivyo mpango wa kudhibiti hili ni kuwavutia wawekezaji kushirikiana pamoja na serikali kuanzisha USAFIRI ambao utakuwa maalumu kwa wanafunzi tu ambao utakuwa na Ratiba za kufika Vituoni kwa muda Elekezi ambapo wanafunzi watatakiwa kuwa vituoni hapo Mfano KITUO CHA TEGETA ( saa 11:40 asubuhi), Kituo cha AFRIKANA (saa 11:50) na kuendelea kwa Wale wanaosoma shule za Mjini Dar es salaam. Hii kwa kiasi kikubwa utapunguza adha hiyo

1719672602121.png
chanzo: MTAA KWA MTAA BLOG

2. MATUMIZI YA NYIMBO KATIKA UFUNDISHAJI
Inaonekana wazi kuwa Masuala ya Nyimbo kama Bongo fleva, Singeli, Amapiano na mfano wa hizi zimekuwa na mvuto mkubwa sana kwa watu wote hivyo ubunifu unatakiwa kufanywa kwa kuwashirikisha Wataalamu wa ndani kutoka TAASISI YA ELIMU TANZANIA ama Walimu wa mashule husika na Kushirikiana kwa pamoja na Wasanii Maarufu kama Diamond, Ali Kiba na Harmonize ili kutumia uwezo na ushawishi wao katika kuandaa mada zinawezekana kuundiwa nyimbo hii itawasaidia wanafunzi kuzirudia rudia hizo nyimbo hali itakayoongeza kumbukumbu yao katika Masomo.

Mfano Teacher Yusuphu amekuwa akitumia njia hii kama inavyoonekana kupitia kiunganishi hiki hapa chini
Chanzo:
View: https://www.instagram.com/reel/C4BmkAKN4AX/?ingsh=bzJ3Zzh6aG9qMTNr

3. MATUMIZI YA SANAA YA MASIMULIZI KATIKA KUFUNDISHIA
Ukitoa uwepo wa masomo mahususi yanayohusiana na Masimulizi kama KISWAHILI, ENGLISH na LITERATURE IN ENGLISH ipo haja sasa Kutumia sanaa hii ya Masimulizi katika kuboresha ufundishaji kwa Masomo yote. Hii itasidia sana kutoka na namna ambavyo kwa sasa jamii imekuwa mstari wa mbele kufuatilia masimulizi mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii, Vipindi vya Televisheni na Redio

4. UFUNDISHAJI WA KUTUMIA TEKNOLOJIA
Tumeshuhudia kukua kwa kasi ya sayansi na Teknolojia hadi kufikia Generation ya Tano (5G) ambapo itatoa intaneti yenye kasi zaid kwa Ufanyaji kazi wa Vitu mbalimbali kama ROBOTI, AKILI MNEMBA na kadhalika yote haya yatasaidia mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi Kuwezesha Matumizi ya akili Bandia (AI) katika kujifunza vitu mbalimbali, Kuunganisha Mifumo mbalimbali wakati wa kujifunza Mfano Matumizi ya PROJECTA, Lakini pia utaboresha uwezekano wa kupata Vitabu na Mambo muhimu ya kujifunza Mtandaoni:

Screenshot_20240629_185747_Chrome[1].jpg

Chanzo: TIE LIBRARY​

5. UBORESHAJI WA MISHAHARA NA MAZINGIRA YA UFUNDISHAJI KWA WALIMU
Walimu ndio nyenzo kubwa katika kuhakikisha Sekta hii inaimarika kwa kuwa wao ndio Chanzo kikuu cha Maarifa kwa wanafunzi sasa kwa umuhimu wao huo mkubwa serikali , jamii na wadau mbali mbali wanapaswa kuwapa heshima kubwa kwa namna wanavyohangaika kuandaa Wataalamu watakao itumikia nchi katika kila eneo. Na katika kuhakikisha hilo niiombe serikali kupitia upya Miongozo yake ili kuweka mishahara minono kwa walimu kwa kazi kubwa wanayoifanya maana ni imani yangu kuwa Mishahara itawapa utulivu wa fikra walimu na kuwafanya wawekeze nguvu kubwa katika Kufundisha kuliko kujiingiza katika biashara ndogondogo zinazokula muda wao wa kuandaa masomo/vipindi

6. KUTOA MIKOPO YA ADA KWA WANAFUNZI WOTE
Tunafahamu kuwa kwa wengi wa watanzania ni watu wenye hali ya kawaida kiuchumi na sio rahisi kwao kuweza kujikimu katika suala la ADA Vyuoni kutokana na ukubwa wake hivyo Serikali kwa kushirikisha wadau mbalimbali ipitie vema BAJETI ZA ELIMU ili kufikia miaka 5 hadi 15 ijayo iwe na mpango mkakati katika hilo
Suala la ADA Linawakwamisha wengi kushindwa Kuendelea na masomo, kusoma bila kuhitimu na pia Kushindwa kusoma KOZI walizokuwa wakizihitaji hivyo kwa kuwalipia ada tutakuwa tumepunguza kwa kiasi kikubwa changamoto hii na kujihakikishia upatikanaji wa Wataalamu wa kutosha nchini kwa maendeleo ya Taifa

7. KUBORESHA MFUMO WA UPIMAJI WA MITIHANI YA TAIFA
Kutokana na Changamoto za kimazingira upo uwezekano mkubwa wa mwanafunzi kushindwa kufanya vema kutokana na hali za kimazingira kama vile Kufiwa na Watu wa karibu siku za mitihani, Maradhi ya Ghafla, Majanga mbalimbali Mfano Mafuriko na kadhalika hivyo Kuliko kurudia mwaka Mzima serikali ingeweka uatartibu mzuri wa kuhakikisha Kuwe na namna nyingine zinashirikiana kwa pamoja na Mitihan ya Taifa katika kupata jumla ya Maksi zote za mtu kuweza kufaulu Mfano Kukusanya na kuzisimamia kikamilifu CA za wanafunzi kwa kuzingatia mitihani ya nje Mfano MOCK na PRE NATIONAL za Wilaya na Mkoa.

Kwa ujumla Maendeleo haya Yanapaswa kufanyika kwa awamu ili yawe na Matokeo chanya maana kuyafanya yote bila mipango madhubuti inaweza isilete mabadiliko ya tunayokusudia. Pia ni muhimu kwa Wanafunzi pia kufahamu jukumu na wajibu wao hasa katika kuwekeza nguvu yao kusoma kwa bidii ili nguvu inayotolewa na SERIKALI, WALIMU, WAZAZI na JAMII kwa ujumla isiende bure maana tumeona baadhi ya wabunge wakitoa malalamiko juu ya matumizi mabaya ya BOOM kwa wanafunzi wnufaika wa mikopo ya BODI YA MIKOPO nchini, Lakini pia wengi wa wanafunzi kuwa watoro mashuleni na kuacha kabisa pasina sababu ya msingi kwa kuwa serikali imeelekeza ELIMU BURE kwa watu Wote.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom