Maboresho TPA yaongeza meli, mizigo

Maboresho TPA yaongeza meli, mizigo

kalacha mateo

Senior Member
Joined
Sep 27, 2021
Posts
119
Reaction score
240
Uboreshaji unaoendelea katika sekta ya bandari nchini umeongeza ufanisi na kati ya Oktoba hadi Desemba idadi ya meli zilizohudumiuwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) zimeongezeka. Msemaji Mkuu wa serikali, Gerson Msigwa alisema jana mjini Dodoma kuwa kipindi hicho meli zilizohudumiwa na TPA zimefikia 555 na kati ya hizo meli 308 zilikua za bahari kuu na 247 zilikua za mwambao sawa na Ongzeko la 9%

Aidha, meli 510 zilihudumiwa katika robo ya kwanza ya mwaka jana kuanzia Julai hadi Septemba na ongezeko hili ni sawa na 16%. Katika kipindi cha kuanzia Oktba hadi Desemba mwaka jana kiwango cha shehena kilichohudumiwa pia kimeoingezeka.

Msigwa alisema uboreshaji wa miundombinu bandari ya Dar es Salaam unaendelea ile kazi ya kwanza ya upanuzi wa miunombinu ya bandari na kuongeza kina kama unayoona kuna mitambo ya kuongeza kina na kazi inaendelea ambapo mpaka sasa imefikia 72%.

Pia serikali inajenga bandari kavu ya kwala umefikia 87%, Bandari ya Tanga maboresho maboresho ya awamu ya kwanza yamekamilika huku awamu ya pili utekelezaji wake ukifika 87% ambao unahusisha uboreshaji wa gati namba moja na namba mbili ambapo mategemeo ni kumaliza changamoto za bandari ya Tanga.
 
Back
Top Bottom