hakuna mpango wa kuboresha daftari la wapiga kura kwa kuwa serekali haina pesa. pengine 2016.WanaJF, mnisamehe kama hili suala limeshaulizwa na kupatiwa ufumbuzi kwani kwa upande wangu katika kupitia humu sijaiona! Nauliza hivi, kama Bunge maalumu la Katiba litapitisha katiba mpya kitakachofuata ni kura ya maoni. Je waTZ tutapiga kura kabla daftari la wapiga halijaongezwa majina ya vijana waliofikisha miaka kumi na minane baada ya kuboreshwa kwa mara ya mwisho? Serikali itakuwa haitendi haki kwa raia wake.
WanaJF, mnisamehe kama hili suala limeshaulizwa na kupatiwa ufumbuzi kwani kwa upande wangu katika kupitia humu sijaiona!
Nauliza hivi, kama Bunge maalumu la Katiba litapitisha katiba mpya kitakachofuata ni kura ya maoni. Je waTZ tutapiga kura kabla daftari la wapiga halijaongezwa majina ya vijana waliofikisha miaka kumi na minane baada ya kuboreshwa kwa mara ya mwisho? Serikali itakuwa haitendi haki kwa raia wake.
Mkuu, kabla ya kufikiri kuhusu daftari la kudumu la wapiga kura, hebu wahi mapema ukajiandikishe kwenye daftari la balozi/wako wa mtaa - au daftari la kata. Hili ndio litatumika katika kupiga kura za serikali za mtaa mwaka huu. Hili zoezi limekuwa ni la siri mno na huenda wengi wasilijue na kukosa fursa ya kuwapiga chini magamba. Kumbuka hapa ndipo magamba huwa wanatuzidi ujanja maana wapo kwenye system.