Maboresho ya elimu msingi na awali

Maboresho ya elimu msingi na awali

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Serikali imeeleza kishindo kingine katika sekta ya elimu baada ya kueleza mwaka huu imepanga kujenga madarasa mapya 9,000 kwa shule za msingi na awali.

Katika mpango huo Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu inatarajia kutumia Tsh Bilioni 250.9 kwa lengo la kuboresha miundombinu katika shule hizo

Hii inaonyesha ni jinsi gani Serikali ya Rais Samia Suluhu inavyopambana na ujinga maana ujinga ndio chanzo cha umasikini Elimu inaendelea kuboreshwa Rais Samia Suluhu anafanikisha elimu bila ada katika mazingira bora.
 
Je taarifa haisemi ataajiri waalimu kiasi gani?
Hayo madarasa yanaboresha elimu yenyewe tu,pasipokua na idadi wiano ya waalimu?
Serikali hii ishauriwe,juhudi za ujenzi,ziende sambamba na kuajiri waalimu.
 
Serikali imeeleza kishindo kingine katika sekta ya elimu baada ya kueleza mwaka huu imepanga kujenga madarasa mapya 9,000 kwa shule za msingi na awali.

Katika mpango huo Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu inatarajia kutumia Tsh Bilioni 250.9 kwa lengo la kuboresha miundombinu katika shule hizo

Hii inaonyesha ni jinsi gani Serikali ya Rais Samia Suluhu inavyopambana na ujinga maana ujinga ndio chanzo cha umasikini Elimu inaendelea kuboreshwa Rais Samia Suluhu anafanikisha elimu bila ada katika mazingira bora.
Mzee hayo sio maboresho ya elimu huo ni ujenzi wa miundo mbinu.
 
Serikali imeeleza kishindo kingine katika sekta ya elimu baada ya kueleza mwaka huu imepanga kujenga madarasa mapya 9,000 kwa shule za msingi na awali.

Katika mpango huo Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu inatarajia kutumia Tsh Bilioni 250.9 kwa lengo la kuboresha miundombinu katika shule hizo

Hii inaonyesha ni jinsi gani Serikali ya Rais Samia Suluhu inavyopambana na ujinga maana ujinga ndio chanzo cha umasikini Elimu inaendelea kuboreshwa Rais Samia Suluhu anafanikisha elimu bila ada katika mazingira bora.
Hivi maboresho ya elimu ni vyumba vya madarsa? Kuna mwaka nchi hii tangu ipate uhuru hapajajengwa vyumba vya madarasa?
 
Hii nchi madarasa na madawati hayatakaa yatoshe bila kufanya udhibiti katika suala la uzazi wa mpango ili watoto wanaozaliwa waendane na kasi ya ukuaji uchumi. Uchumi unaokuwa kwa 7% ni mdogo sana kwa nchi maskini kuweza kuhimili kasi kubwa ya ongezeko la watu.
 
Mkumbusheni pia kwamba, lipo lundo la watoto hadi wanamaliza darasa la saba hawajui kusoma na kuandika! Mmwambie kuwa, hili ndilo la kutafutia dawa kwa haraka kuliko haya majengo!
 
  • Kwani walikopa kiasi gani kwaajili ya madarasa?
  • Walisema kufikia lini yangekuwa yamekamilika?
  • Hizo 250bn zinatoka wapi?
  • Tozo zimefikia ngapi mpaka sasa?

Green city 3 zimefikia wapi?
Kule kwa Nnaayep, walisambaza darasa moja juu chini udongo, milango kama yote

Tunakusanya 2. trillion sio, ngoja tuone ngonjera itatamatika vipi!
 
Nyinyi ndiyo mnampotosha. Ujenzi mpaka lini? Watendaji wanajua ujenzi ndiyo sehemu ya kulia hela za umma. Toa ajira kwa walimu pia
 
Ajira ndugu za walimu zikitoka ndio uje ufungue uzi hzo mambo mengine achana nazo madarasa ya nn wakati miembe hipo mingi tyuu ni bora wakae chini ya miembe hila wawe na walimu at least wakihitimu elimu ya msingi wajue kusoma yatosha kuliko kukaa madarasan bila walimu watahitimu awajui kusoma litakua janga kwa taifa langu
 
Back
Top Bottom