Aballhalim
New Member
- Jul 18, 2022
- 2
- 1
UTANGULIZI
Awali ya yote nipende kumshukuru Mwenyezimungu Aliyenipa afya na fikra za kuchangia story of change ambayo inaweza kuibua mijadala mbalimbali yenye kuleta mchango kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Awali nilishiriki katika mjadala uliowekwa na JamiiForums katika mitandao ya kijamii wenye tittle "UNGEWEZA KUONDOA SOMO LOLOTE UNGEPENDA KUONDOA SOMO GANI!?"
Nilishikiri mada hiyo na kupendekeza kuondolewa masomo kadhaa kutokana na kutomjenga mwanafunzi kukabili maisha ya mtaani (Kujiajiri) baada ya kuhitimu!
Nichukuwe fursa hii kupendekeza kwa serikali kuufanyia maboresho mfumo wa elimu ili uweze kuwapa wahitimu ujuzi, maarifa, ubunifu, udadisi na wasio na fikra tegemezi.
Maboresho hayo yafanyike kwenye mitaala ya elimu (silabasi) na kwenye baadhi ya masomo!
MABORESHO KWENYE MITAALA YA ELIMU (SILABASI)
Mitaala yetu ya elimu kwakiasi imeshindwa kumjenga mwanafuzi kuweza kukabili maisha ya mtaani/kujiari baada ya kuhitimu. Hii ni kutokana na mitaala hiyo kutojikita kwenye uhalisia wa maisha anayokwenda kuyakabili mwanafunzi mtaani.
SOMO LA KIINGEEZA (ENGLISH)
Mfano wa wazi kwenye somo la kiingereza ambalo ni muhimu na fursa ya kujiari kwa maisha ya Tanzania ya leo, somo hili limekuwa likisomeshwa tangia shule za msingi hadi sekondari lakini silabasi yake imekuwa haimjengi mwanafunzi kuwa na ujuzi wa lugha hiyo wa kumuwezesha kuitumia katika mawasiliano kiufasaha, lugha ambayo amekuwa akiisoma kwa zaidi ya miaka 10! Kwa kulinganisha na Silabasi ya English course ya mtaani ambayo humchukuwa mwanafunzi kuanzia miezi sita hadi tisa kuweza kuwa na ujuzi wa lugha hiyo na pengine hata kuwa fasaha kwenye lugha husika!
SOMO LA HISTORIA
Somo hili limejikita Zaidi kuisoma historia za nchi nyengine na kwa uchache historia ya nchi yetu, lakin elimu hiyo haituongezei maarifa wala ujuzi wa kuja kukabiliana na maisha ya baadae walau kuwa fursa ya ajira kwa taifa letu, tungejikita Zaidi kutoa elimu ya historia ya kwetu mfano mji wa Kilwa, Bwagamoyo na Zanzibar tangia shule za msingi na kwa uchache historia za nchi jirani, kwakiasi tungeongeza ujuzi, maarifa na fursa za ajiari kwani historia za miji hii maarufu zimekuwa kivutio kikubwa kwa watu kutoka nje ya taifa letu, lakini cha ajabu historia za miji hiyo zimekuwa zikisomwa na watu kutoka nje ya taifa letu na kutungiwa vitabu mbalimbali na kuwa fursa kwao kwa kuuza vitabu sehemu mbalimbali, vitu ambavyo vingeweza kufanywa na wahitimu wetu!
SOMO LA CIVICS (GENERAL STUDY)
Somo hili limejikita kujenga taifa lenye thamani katika nanja mbalimbali lakini lengo limekuwa gumu kufikiwa pengine labda mtaala huo haujajitoshelezi. Mwanafunzi husomweshwa filosofia za watu toka nje ya bara na taifa letu ambazo haziendani na uhalisia wa maisha yetu, kimsingi inakuwa vigumu kumuongezea maarifa badala yake humuacha na fikra tegemezi, ni vyema tungetafuta namna ya kutengeneza wanafalsafa wetu kwa kuwajengea msingi hadi vyuo vukuu.
Tungeanzisha masomo ya Siasa yanayoendana na uhalisia wetu, jamii ingeweza kujua wajibu wa viongozi na tungezalisha viongozi wazuri, wawajibikaji, wenyeuwezo wa kujenga hoja wasiokuburuzwa kifkra na viongozi wenye nia ovu kwao! Masomo ya kumuandaa mwanafuzi kuwa na tabia njema, mzalendo, muwajibikaji, na mfano wa hayo yangepewa kipaombele na kuandaliwa mfumo mzuri wa utolewaji ili tujenge jamii itakayolipa thamani taifa letu.
SOMO LA GOGRAFIA
Kama nchi tunavingi vya kuifunza jamii kuyakabili maisha kupitia somo hili. Mtaala wa elimu umetawaliwa na kuzisoma shughuli za kiuchumi na kijamii za nchi za wenzetu na kwa uchache za nchini kwetu, jambo ambalo linampa wakatimgumu mhitimu baadae, elimu ya shughuli za kiuchumi hutolewa kama vile kilimo, utalii, uchimbaji wa madini, uvuvi, ufugaji na kadhalika, nchi yetu inahazina nyingi za kiuchumi kama jamii ingepata mfumo bora wa elimu ya kuzitumia hazina hizo unaoendana na uhalisia wetu tungetengeza jamii yenye ujuzi, maarifa, na kuzalisha na tungeweza kupunguza tatizo la ajira.
SOMO LA KISWAHILI
Kiswahili ndio lugha mama ya taifa, ipo haja ya kuwekeza nguvu kubwa kuhakikisha tunaikuza na kuwa na wataalam wengi wa lugha hii, tunapaswa kuwa na mtaala bora wa kuifundisha lugha hii. Kwakiasi tumefanikia pakubwa kwenye somo hili kwani wanafunzi wengi huweza kujengewa ujuzi na uwezo wa kusoma na kuandika ambao unawasaidia kwakiasi kikubwa kwenda kyakabili maisha baada ya kuhitimu, maboresho Zaidi ya kimtaala yafanyike katika kuhakikisha tunatengeza wataalamu wa Kiswahili na kukikuza.
MASOMO YA SAYANSI, HESABATI NA TEKNOLOJIA
Kwa ulimwengu huu wa utandawazi, jamii inahitaji sana elimu ya sayansi na teknolojia ili kupunguza mzigo wa ukosefu wa ajira, Masomo ya matumizi ya compyuta, programing, social network digital, online development digital na mengineyo mfano wa haya yanayoendana na uhalisia wa soko la kwetu yangeekewa mfumo mzuri na kutolewa japo msingi wake ili imuongezee kijana hamasa ya kujifunza Zaidi. Masomo mengine kama Kemia, Phizikia na Baiolojia yamekuwa mfano mzuri husomeshwa tangia msingi wake na humpa hamasa mwanafunzi kujifunza Zaidi na kuwa na ndoto nayo.
Kwa mifano hii ni wazi kwamba mfumo wetu wa elimu na baadhi ya silabasi kwenye masomo zimepitwa na wakati au haziendani na uhalisia wetu, hivyo zinahitaji kurekebishwa au kubadilishwa! marekebisho haya yaanzie shule za msingi.
MASOMO MENGINE YA KUONGEZWA KATIKA MTAALA WA ELIMU
Mtaala wa elimu ungeongezewa masomo yatakayojumuisha nadharia na vitendo kuanzia shule za msingi, sekondari, hadi vyuo vikuu! Elimu itoe fursa ya kujua kusoma, kuandika, mazingira, ujasirimali ujuzi na maarifa katika fani mbalimbali kwenye kazi za mikono kama vile uvuvi, seremala, kilimo, ufugaji, ujenzi na kadhalika ili kuweza kujijengea msingi wa mahitaji binafsi ya mtu mmoja mmoja, familia. Elimu ya ujuzi ndio msingi mkubwa wa mafanikio kwa jamii!
HITIMISHO
Ushauri kwa wizara husika iunde mfumo utakaomuewezesha mwanafunzi kuyakabili maisha ya baadae kwa level ya elimu aliofikia, hata yule aliefeli darasa la saba anufaike na elimu hiyo mtaani japo kwa uchache, elimu ya kidato cha sita kwakiasi haitufanyi kuweza kuyakabidi maisha ya mtaani (kujiari), Hili ni tatizo kwani hutupotezea miaka mingi kujifunza tusiyoyahitaji kwajili ya kuyakabili maisha ya baadae.
mfumo tulionao sasa unawapa fursa wahitimu wa chuo tu ndio wanaouwezo kwakiasi kuyakabidi maisha ya uraiani, elimu ngazi ya chuo ndio hujenga ujuzi na maarifa, mbali na elimu hiyo mfumo wa masomo unawakaririsha wanafunzi (content) ambazo haziwaongezei ujuzi wala maarifa! Naamini kuanzishwa kwa mfumo wa aina hii utaleta chachu ya maendeleo kwa jamii na taifa.
Karibu katika mjadala huu uchangie na kupiga kura

Upvote
0