Kimaro Robbie
New Member
- May 1, 2023
- 3
- 3
Mtaala ni mpango wa masomo ambao hutumiwa na shule au mfumo wa elimu kuamua ni nini cha kufundishwa na jinsi ya kufundisha. Tanzania inatumia Mtaala wa Elimu ya Msingi na Mtaala wa Elimu ya Sekondari, ambayo huwa na malengo ya kufundisha wanafunzi ujuzi, mawazo na maadili wanayohitaji kukua na kuwa wajumbe wema wa jamii.
Katika nchi yetu ya tanzania mitaala inayotumika haikidhi mahitaji halisi ya jamii ya kitanzania kwa sababu mitaala inayofundishwa mashuleni na Vyuoni haijalenga katika kuzalisha watanzania kuweza kujitegemea wenyewe baada ya kumaliza elimu ama fani wanazosomea Bali kuitegemea serekali kwa kiasi kikubwa kuwapa ajira Jambo ambalo kwa miaka ya karibuni limekuwa gumu kwa serekali kutoa ajira kwa watu wote wanaomaliza vyuo vikuu na vya Kati hivyo wasomi kubaki wanalaumu kwa sababu mitaala iliwaandaa wao kwa ajili ya kuajiriwa na sio kuwapa ujuzi na uthubutu wa kujiajiri
Mitaala inayotumika katika nchi yetu inazo changamoto ambazo watunga Sera pamoja na wadau wa elimu inawapasa kuangalia ili kuweza kuandaa mitaala ambayo itaendana na maisha halisi ya mtanzania na kutoa ujuzi na maarifa yatakayomwezesha mtanzania kuweza kujitegemea na kuchochoea mabadiliko chanya katika jamii changamoto hizo Ni Kama ifuatavyo;
1. Mfumo wa elimu unazingatia sana kufaulu mitihani kuliko kutoa maarifa ya uhakika
2. Mitihani haizingatii ujuzi mpya unapozalishwa au msisitizo wa maendeleo ya vipaji vya wanafunzi
3. Mitaala pia ina mapungufu katika kuzingatia maendeleo ya teknolojia na kujenga ujuzi wa kitaalam katika kada za kisasa
4. Kuna upungufu mkubwa wa ushiriki wa wazazi na wanajamii katika maisha ya shule na utoaji wa elimu
5. Mitaala haitoi nafasi za kutosha za kuendeleza stadi za kujifunza za wanafunzi
6. Mitaala ya Tanzania hairuhusu ushindani na nchi nyingine duniani
Suala la kuboresha mitaala Ni Jambo muhimu Sana kwa maendeleo ya nchi yetu hasa katika kuzalisha taifa lenye wasomi ambao watalisaidia taifa hivyo Kuna hatua mbalimbali za kufuata ili kuhakikisha Mitaala inayotengenezwa Ina sadifu Yale ambayo mtanzania wa kawaida anayaishi katika jamii Yake Kama ifuatavyo;
Kwanza kabisa, tutahitaji kufanya utafiti wa kina juu ya mitaala ya elimu iliyopo sasa. Hii inahusisha kukusanya taarifa kuhusu mitaala hiyo, kufanya tathmini ya kina juu ya mambo yaliyofanya vizuri na yasiyofanya vizuri, na pia kutambua mahitaji ya wanafunzi wako na jamii kwa ujumla.
Baada ya kupata taarifa hizi, tunaweza kuanza mchakato wa kubadili mitaala. Hii inahusisha maeneo ambayo yanaanguka na kuyaboresha, kupendekeza maudhui mapya kulingana na mahitaji ya sasa na ya baadaye ya wanafunzi na jamii, na kuboresha jinsi gani maudhui hayo yanafundishwa.
Sababu mitaala ni jambo la kitaifa, lazima kushirikiana na wadau wengine ambao wanajua zaidi kuhusu hilo. Hii inaweza kuwa na wataalam wa elimu, viongozi wa serikali, wanafunzi, walimu, na wazazi. Kwa kushiriki na wadau wengine, tutakuwa na fursa ya kukusanya maoni tofauti, kufikia makubaliano kuhusu mabadiliko yatakayotekelezwa, na kupata uungwaji mkono wa wasimamizi na wadau wengine.
Maboresho ya mitaala yetu yanapaswa yafanyike katika maeneo yafuatayo katika kuzalisha wasomi wenye maarifa na ujuzi wa kulisaidia taifa :
1. Kuimarisha maandalizi ya walimu: Wizara ya Elimu inapaswa kuwekeza katika kuimarisha maandalizi ya walimu, kuhakikisha kuwa wanapata mafunzo ya kutosha na ujuzi wa kujifunza na kufundisha wanafunzi juu ya stadi Bora za maisha namna ya kujitegemea pale wanapo hitimu Yale wanayosomea mashuleni pia kuwajengea wanafunzi hali ya kujiamini katika kujitegemea na kutumia ujuzi wao wenyewe
2. Kubadilisha muundo wa mitihani: Mitaala ya Tanzania inazingatia sana kufaulu mitihani, hivyo mtihani haupimwi kwa kiwango cha maarifa bali kwa kiwango cha kukariri. Inapaswa kufanyika mabadiliko ili mitihani iweze kupima maarifa halisi ya mwanafunzi na si kukuza tabia ya kukariri,kwa kufanya hivi itasaidia wanafunzi kutumia ujuzi walio upata mashuleni katika kujinufaisha na kujitegemea wenyewe.
3. Vifaa bora vya ufundishaji: Wizara ya Elimu inapaswa kuwekeza katika vifaa vya kufundishia na kujifunzia kama vile vitabu, kompyuta, DVD, na vifaa vingine vya teknolojia ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu nzuri, ya hali ya juu inayokidhi mahitaji yao,vifaa hivi vitajenga uelewa wa kutosha kwa wanafunzi juu ya Yale wanayofundishwa mashuleni na kuyaleta katika maisha ya kawaida.
4. Kurekebisha maudhui ya mtaala: Mtaala wa elimu unahitaji kurekebishwa ili kujumuisha mabadiliko ya kisasa, mahitaji ya jamii, na miaka ya hivi karibuni. Kuna mambo mengi ya kujifunza ambayo hayapatikani katika mtaala wa sasa, kwa hivyo ni muhimu kurekebisha ili kuongeza maarifa muhtasari yanayofaa,mfano baadhi ya Muhtasari ambayo haipo katika mahitaji ya Sasa Inabidi kuondolewa
5. Kuanzishwa kwa masomo ya ujasirimali ,kilimo ,ufugaji na uvuvi kulingana na mahitaji na rasilimali zipatikanazo katika maeneo husika wizara inabidi ianzishe masomo ambayo yatawasaidia wanafunzi pale wanapo maliza elimu kuweza kujitegemea mfano katika maeneo yote ambapo Ni wakulima wanafunzi wafundishwe stadi Bora za kilimo,katika maeneo ya ufugaji pia wafundishwe ufugaji Bora na wakisasa vivyo hivyo katika uvuvi ,uchimbaji wa madini kwa kufanya hayo wanafunzi wataweza kuwa na uwezo wa kutosha kujitegemea na kujenga Pato lao na taifa kwa ujumla.
6. Matumizi ya tehama mashuleni:kutokana na mabadiliko makubwa ya ya sayansi na tehama wizara ya elimu inapaswa kuhakikisha kuwa inaendana na mabadiliko haya katka mfumo wa elimu kwa kuanzisha somo la tehama na kuliwekea mkazo katika shule zote za umma na binafsi hii itasaidia Sana kujenga uelewa kwa wanafunzi kutumia ujuzi huo vizuri katika kutafuta fursa mbalimbali zilizopo katika tehama
Kwa kuhitimisha: Kuna kila sababu ya kufanya maboresho katka mfumo wetu wa elimu ili kuhakikisha taifa linapata wasomi ambao wanaweza kuliendeleza taifa kwa kutumia ujuzi walionao vizuri katika nyanja zote Kama kilimo, viwanda, usanifu, madini, ufugaji hii itasaidia wananchi wengi kuwa na uwezo wa kujiajiri pia kuongezeka kwa Pato la taifa pia itasaidia zabuni nyingi za serekali na watu binafsi kupewa wazawa hivyo basi kwa maendeleo ya taifa Kuna umuhimu mkubwa sana wa mitaala kubadilishwa kuendana na mahitaji halisi ya mtanzania.

Upvote
1