Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 105
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango juu ya Matokeo ya utekelezaji wa Serikali ya awamu ya tano katika Sekta mbalimbali, miongoni mwa Sekta zilizoelezwa utekelezaji wake ni Sekta ya Mawasiliano.
Ambapo Ripoti hiyo inaeleza kuwa kwenye Sekta hiyo yamefanyika maboresho kadha wa kadha ikiwemo Ujenzi wa Mkongo wa Taifa ambao unaelezwa kupunguza gharama za kupiga simu za mkononi kutoka Shilingi 349 kwa dakika mwaka 2010 hadi Shilingi 70 kwa dakika mwaka 2020.
Aidha maboresho mengine kwenye Sekta hiyo ni pamoja na matumizi ya Mifumo mipya ya Mawasiliano kama vile Mfumo wa pamoja wa ukusanyaji Kodi na Maduhuli ya Serikali (Government Electronic Payment Getaway- GoPG), TTMS(Teletraffic Monitoring System).
Mifumo hiyo imewezesha kuongeza Mapato ya Serikali kwa zaidi ya Shilingi Billioni 100 hadi kufikia Januari 2020.
Ripoti hiyo pia inaeleza kuhusu ujenzi wa Minara 704 kwa gharama ya Shilingi Billioni 151.97 , ambapo Minara hiyo imewezesha huduma ya Mawasiliano kufikia wananchi kwa asilimia 94.