i_denyc
New Member
- Jun 6, 2023
- 4
- 8
UTANGULIZI
Mapinduzi matatu ya viwanda yaliopita yalileta maendeleo ya kiteknolojia ambayo yalibadilisha kwa kiasi kikubwa hali ya kiuchumi na kijamii, hivyo kulihitajika marekebisho ya kisheria yanayolingana ili kushughulikia changamoto na fursa mpya zilizojitokeza kwenye jamii. Sheria za kazi, sheria za umiliki, sheria za mawasiliano nk zilitokana na mapinduzi haya matatu ya viwanda.
Mwaka huu bunge la Tanzania lilipata ugeni wa roboti Yunus ambae alimpokea waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari Nape Nnauye. Hii inaashiria ya kwamba mapinduzi ya nne ya viwanda (4IR) yamekuja na teknolojia ambayo inabadilisha jinsi tunavyoishi, kufanya kazi, na kuhusiana sisi kwa sisi. Teknolojia ya akili bandia, roboti, zinahitaji mfumo wa kisheria unaoweka mazingira yanayofaa. Uvumbuzi katika 4IR ni ufunguo wa mafanikio, inafaa kuzingatia kwamba mfumo wa udhibiti hauna nafasi katika ajenda ya 4IR na lengo la maboresho yoyote ya kisheria yawe kuunda mfumo wa sheria shindani ambao unazingatia mabadiliko yaliyoletwa na mapinduzi mapya ya viwanda.
Mapinduzi matatu ya viwanda yaliopita yalileta maendeleo ya kiteknolojia ambayo yalibadilisha kwa kiasi kikubwa hali ya kiuchumi na kijamii, hivyo kulihitajika marekebisho ya kisheria yanayolingana ili kushughulikia changamoto na fursa mpya zilizojitokeza kwenye jamii. Sheria za kazi, sheria za umiliki, sheria za mawasiliano nk zilitokana na mapinduzi haya matatu ya viwanda.
Mwaka huu bunge la Tanzania lilipata ugeni wa roboti Yunus ambae alimpokea waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari Nape Nnauye. Hii inaashiria ya kwamba mapinduzi ya nne ya viwanda (4IR) yamekuja na teknolojia ambayo inabadilisha jinsi tunavyoishi, kufanya kazi, na kuhusiana sisi kwa sisi. Teknolojia ya akili bandia, roboti, zinahitaji mfumo wa kisheria unaoweka mazingira yanayofaa. Uvumbuzi katika 4IR ni ufunguo wa mafanikio, inafaa kuzingatia kwamba mfumo wa udhibiti hauna nafasi katika ajenda ya 4IR na lengo la maboresho yoyote ya kisheria yawe kuunda mfumo wa sheria shindani ambao unazingatia mabadiliko yaliyoletwa na mapinduzi mapya ya viwanda.
Chanzo, google (Millard Ayo)
Zifuatazo ni ishara za 4IR kwenye nyanja mbali mbali zinazoonyesha mapungufu kwenye sheria zetu na namna tunavyoweza kuziboresha.
1. AFYA
Kumekuwa na utoaji huduma ya afya kwa njia ya mfumo wa teknolojia ya mtandao bila ya mgonjwa wala mtoa huduma kuwa sehemu moja (telemedicine). Na pia utambuzi wa magonjwa kwa kutumia akili bandia kupitia uchambuzi wa data na picha za kiafya kuboresha usahihi na kasi ya utambuzi wa magonjwa hospitalini. Hii hupunguza makosa ya watabibu katika utambuzi wa magonjwa mbalimbali kama saratani.
Wataalamu wakitoa tiba kwa kutumia teknolojia ya kisasa. Chanzo, tovuti ya Truevision
MAPUNGUFU YA SHERIA: Hizi ni huduma mpya na zenye gharama kwa watanzania walio wengi, Sheria ya mfuko wa taifa wa bima ya afya sura ya 395 ya 2015 hazijajumuisha huduma za kisasa kama hizi kwenye faida za mfuko wa bima ya afya hivyo kupelekea wagonjwa wengi kutokuzimudu na kukosa huduma ya afya.
MABORESHO: Kutengeneza utaratibu wa kisheria kuzijumuisha huduma za kisasa kwenye mfuko wa taifa wa bima ya afya. Na pia ni wakati sahihi wa Sheria ya Afya kwa Umma ya mwaka 2009 na Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba ya mwaka 2003 kuboreshwa ili kuweka miongozo maalumu ya kutoa huduma za "telemedicine" kuhakikisha ubora na usalama. Hii ni pamoja na kudhibiti maadili ya kitaaluma, usalama wa taarifa na viwango vya utoaji huduma ili kuendana na mabadiliko ya sayansi.
2. MAWASILIANO
Watanzania wengi wanamiliki simu janja hivyo kumeongezeka kwa majukwaa ya kidijitali na mitandao ya kijamii imekuwa njia kuu za mawasiliano na usambazaji wa habari kwa watu wengi, huku mitandao ya kijamii kama vile Facebook, X, Jamii Forums na Instagram kuwa vyanzo vikuu vya mawasiliano na burudani. Hii imewapa watu binafsi uwezo wa kuunda na kushiriki maudhui mbalimbali.
MAPUNGUFU YA SHERIA: Maudhui ya mitandao ya kijamii yanasimamiwa na Sheria na. 2 Taarifa ya Serikali na. 133 (EPOCA) ambayo ipo chini ya Wizara ya mawasiliano. Hii inapelelekea wizara kukandamiza maudhui ya mtandaoni na kuzuia uhuru wa watu wa kujieleza ambayo ni haki ya kikatiba.
MABORESHO: Kuzingatiwa kwa viwango vya kimataifa vya "Global Data Protection Regulations" kutumika katika uboreshaji ya Sheria ya Mawasiliano ya Kieletroniki na posta ya mwaka 2010, Sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 na pia kuwe na miongozo madhubuti ili kuhakikisha watanzania wanakua na faragha, ulinzi wa data pamoja na usalama wa mtandaoni.
3. BIASHARA
Kutokana na kuongezeka kwa majukwaa ya kidijitali kumekua na ongezeko la maduka ya mtandaoni, malipo ya mtandaoni na mikopo ya kidijitali. 4IR inaahidi kuleta mabadiliko katika sekta ya benki na jinsi fedha inavyofanya kazi. Tayari benki kuu ya Tanzania inaendelea kutafiti matumizi ya fedha za kidijitali.
Tangazo la BOT kwa umma. Chanzo, tovuti ya bot.go.tz
MAPUNGUFU YA SHERIA: Sheria ya hakimiliki na hakishiriki namba 7 ya mwaka 1999 sura ya 218 inayosimamia haki miliki na alama za biashara hazijafanyiwa maboresho kuendana na kasi ya uvumbuzi hivyo kupelekea wamiliki kupata changamoto ya kuzilinda kazi zao mitandaoni. Na pia hakuna sheria inayowalinda wateja dhidi ya taarifa zinazokusanywa na watoa huduma mtandaoni.
MABORESHO: Ili kuweka mazingira mazuri ya ushindani wa kibiashara katika zama za 4IR, Sheria mpya yenye muongozo wa mfumo wa ukaguzi wa hakimiliki na alama za biashara mitandaoni ili kulinda haki ya uchumi ya wafanyabiashara na watumiaji wa huduma mitandaoni. Sheria ya usajili wa biashara na wakala wa leseni sura ya 217 ziwatambue watoa huduma wote kwa njia ya mtandao ili kuwahakikishia ulinzi watumiaji na kushughulikia masuala ya ulaghai mtandaoni.
4. ELIMU
Kumeibuka mabadiliko ya mbinu za kufundishia kama ulimwengu pepe na "e-learning". Taasisii za elimu ya juu zinatambua manufaa ya programu za elimu mtandaoni, hasa kuhusu hitaji la kuendelea katika mazingira yanayokua ya kidijitali, kwa mfano VR na AR hutumika kutoa uzoefu wa kujifunza kwa vitendo kwa wanafunzi wa udaktari na uhandisi vyuoni.
MAPUNGUFU YA SHERIA: Sheria zetu za elimu zimepitwa na wakati na kulenga ufundishaji wa darasani pekee. Sheria ya Elimu Sura ya 353 marejeo ya mwaka 2002 na Sheria ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi Sura ya 129 hazina kanuni ya kusimamia mtaala wa "e-learning” wenye miongozo ya kina kuhusu viwango vya ubora wa elimu na kuusimamia mtaala wa elimu na mafunzo mtandaoni.
MABORESHO: Sheria ya Elimu Sura ya 353 iongezwe kufungu cha sheria kitakachosimamia elimu ya mtandaoni na mafunzo ya mbali itakayoweka miongozo ya kina kuhusu viwango vya ubora wa elimu na kuusimamia mtaala wa mafunzo ya teknolojia na ujuzi wa 4IR kwenye elimu ya juu.
- Kupoteza fursa za kiuchumi
- Udukuzi na wizi wa mtandao
- Ukosefu wa ajira kwa vijana
- Kushuka kwa viwango vya usalama mtandaoni
- Kupitwa na wakati kama taifa
Kwa ujumla, wito wangu kwa watunga sheria Tanzania hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko makubwa yanayoletwa na 4IR ni muhimu sana kwa taifa letu kujiandaa na changamoto na fursa mpya zinazotokana na maendeleo ya teknolojia kwa kuboresha Sheria mama (Katiba). Tukifanya hivyo Tanzania itaendana na mabadiliko ya 4IR, kukuza uchumi wa kidijitali, na kuhakikisha wananchi tunapata fursa sawa katika teknolojia inayobadilila kwa haraka.
Attachments
Upvote
3