Machache kuhusu Isaac Newton

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Isaac Newton:

Isaac Newton (25 Desemba 1642 – 20 Machi 1727) alikuwa mwanahisabati, mwanafizikia na mwanateolojia kutoka nchi ya Uingereza.

Anakumbukwa duniani kote kutokana na michango yake mbalimbali katika sayansi.

Ndiye aliyegundua tawi la kalkulasi (sambamba na Leibniz), sheria za mwendo na ya uvutano (gravity).

Mchango mwingine wa Isaac Newton upo katika nadharia ya mwanga, akitumia prisma kuonyesha jinsi rangi zinazounda mwanga (kama zinavyoonekana kwenye upinde wa mvua) zinavyotokea.

Alichangia pia astronomia kwa kuboresha darubini ya kuakisia (darubini akisi) iliyoleta matokeo mazuri. Alitambua ya kwamba kanuni za mvutano zinatawala pia mwendo wa sayari. Alitunga ramani ya nyota kufuatana na tafiti za Flamsteed.

Elimu na imani
Newton alipata shahada yake ya kwanza mwaka 1665 na ile ya uzamili mwaka 1668.

Kwa kuwa alizaliwa katika familia ya Kianglikana, alitumia muda mwingi kufanya utafiti wa Biblia na theolojia pia. Alilenga kupatanisha elimu ya sayansi na imani yake. Aliandika "Graviti inaeleza miendo ya sayari lakini haiwezi kueleza ni nani aliyeanzisha miendo yao. Mungu anatawala mambo yote na yaliyopo na yanayoweza kuwepo".

Tarehe 10 Desemba 1682 alimuandikia Richard Bentley: «Siamini ulimwengu unaweza kuelezwa na sababu za maumbile tu, bali nalazimika kuuona kama tunda la hekima na ubunifu vya mmoja mwenye akili». Hata hivyo, yeye binafsi hakukubali mafundisho juu ya Utatu wa Mungu.

Hayo ni machache tu.
View attachment 1072487
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…