Machache kuhusu kabila la Mumuila nchini Angola

Echazzy

Member
Joined
Jan 20, 2018
Posts
65
Reaction score
67
Pichani ni kabila la Mumuila kutoka nchini Angola Kabila hili lina urembo wa aina yake na wa kipekee haswa.
Wanawake katika kabila hili husiliba nywele zao na aina fulani ya msago wa rangi nyekundu mithili ya samli mafuta haya wenyewe huyaita ‘Oncula’ Halafu huchanganya na mafuta mengine kutoka kwenye mti maalumu mitishamba na kinyesi cha ng’ombe kilicho kaushwa vizuri.

Wengine hupamba nywele zao kwa shanga zenye rangi tofauti au huzivika mabaki ya tondo pia hunyoa sehemu ya mbele ya vichwa vyao kama alama ya urembo zaidi Misokoto yao mirefu yakuvutia huitwa Nontombi. Wanawake wa mumuila husuka misokoto kati ya minne hadi sita lakini mila yao huwataka kusuka mitatu tu pindi kuwapo na msiba ndani ya familia.

Shanga nyingi shingoni mwao huanza kuvaliwa na wanawake wa kabila la Mumuila pindi wawapo ndani ya ndoa shanga hizo kwa lugha yao huziita Vilanda. Kabla hawajaolewa huvaa shanga nyingi za rangi ya manjano shingoni mwao wanaziita Vileka na msichana kigoli haruhusiwi kuzivua na atapaswa kulala nazo mpaka pale atakapoolewa.

 
Khaa hao chawa si hataree
 
Harafu ndio mtuambie wazungu waache kuja kutalii sio kweli wanaenjoy africa na kupunguza stress [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hii picha kama wanacheza chuchuma ya vany[emoji126][emoji126][emoji126][emoji126][emoji126][emoji126]
 
Duuuuuuu dunia na Maajabu yake
 
Hayo mamzigo shingoni na kichwani mila ingenishinda
 
Je, wanaoga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…