Kiufupi mechi ilikuwa nzuri na ya kuvutia hasa kwa pande zote mbili yaani Simba na Dynamos.Sharaf shiboub kiungo kutoka Sudan kama ataendelea na performance hii basi tutamsahau kabisa James kotei kwangu sharaf nampa alama 8/10, Tairone da Silva beki huyu kutoka Brazil kiufupi ametulia hana papara sana,anapiga pasi zinazofika sehemu sahihi ila mipira ya juu bado changamoto huyu nampa alama 8/10 pia,shomari kapombe bado yupo ktk ubora kwangu nampa 9/10,kakolanya ni kipa mzuri tatizo hazungumzi na mabeki wake hasa ktk uokoaji wa krosi au mipira ya Kona yeye nampa alama 6/10, Paschal Wawa yupo vizuri sana ila mipira ya juu bado tatizo kwake,mzamiru nampa 7/10, Mohammed Hussein nadhani performance yake ya leo itamfanya kocha kuumiza kichwa kuhusu nani aanze kati yake na Gadiel tatizo lake hajui muda sahihi wa kupiga krosi hivyo nyingi zinapotea huyu nampa 9/10,Deo kanda ni winga mzuri sana ila ana mambo mengi ambayo sio muda wote yanahitajika pia siamini kwa muda wote aliokaa mazembe kama anashindwa kujua kuwa ukiwa ktk eneo gumu la kufunga kutokea pembeni,ni lazima utoe v pass yeye alilazimisha huyu nampa 7/10, Francis kahata performance nzuri sana hapa nampa 8/10,meddie kagere bado yupo ktk peak leo nampa 9/10,Gerson fraga huyu sub yake ilikuja kutuliza mashambulizi ya wapinzani ukizingatia hakuwa na mambo mengi sana japo bado kidogo alikosa confidence Ila nampa 7/10,cleotus chama bado ni mzuri ila anapooza sana mashambulizi leo nampa 7/10,miraji, Rashid juma,ndemla na Kennedy juma kwa muda mfupi waliocheza bado naona ni msaada mkubwa kwa timu hawa nawapa 7/10.