Machache Kuhusu USA

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
Ndilo Taifa lenye mchanganyiko wa watu wa kila Taifa, Kabila na Jamaa Kuliko mataifa mengine yote duniani ikiwa na jumla ya wakazi zaidi ya milioni 320. Wajuzi wa elimu ya jamii wanasema huenda hii ndio sababu ya kuwa na ukarimu sana kwa wageni wakiamini kila mtu duniani huenda ni 'ndugu yao' Hii pia imeifanya Marekani kutokua na lugha rasmi ya kienyeji inagwa yasemekana 80% huwasiliana kwa Kiingereza


2. Moja ya Kazi Ngumu zaidi ni Urais ambapo kati ya Marais 44 wanne wameuawa (Lincoln, Garfield, McKinley and Kennedy were assassinated) wakishika nafasi hiyo huku wengine wanne wakifa kifo cha kawaida (natural death)



3. Jeshi la Anga la Marekani (Air Force) ndilo kubwa kuliko yote duniani


4. Bendera ya Marekani ina Jumla ya Nyota 50 Zinazowakilisha majimbo (States) ya nchi hiyo na misari (Stripes) 13 inayowakilisha Himaya za Muingereza (British Colonies) ambazo zilijitangazia Uhuru na kuwa Majimbo ya kwanza kabisa kwenye Muungano wa Marekani (USA).


5. Kisiwa cha Rhode ndicho kidogo kabisa miongoni mwa Majimbo ya Marekani Huku Alaska ambayo haipakani na majimbo mengine ndilo jimbo kubwa kuliko yote, ingawa tena Rhode ina watu wengi kuliko Alaska, huku jimbo la Montana likiwa na Ng'ombe wengi kuliko idadi ya watu

6. Alama ya Ndege Mtukuka Taifa la Marekani ni Ndege aina ya Tai (Bald Eagle) Likimaanisha Taifa lenye nguvu na Kasi Duniani kama alivyo ndege Tai.....


7. Hadi Mnamo mwaka 1950, ni chini ya 5% tu ya watoto walizaliwa bila wazazi waliooana (Married Couples), hadi hii leo yasemekana idadi hiyo imeongezeka hadi kufikia 40%.

8. Utafiti wa hivi karibuni unaonesha kuwa karibu nusu ya wamarekani (47%) Huenda wakapoteza ajira zao kutokana na mapinduzi ya Komputa, Roboti na nyanja nyingine za teknolojia
 
Hilo taifa Mganga wao sijui ni Nan

au serikali yao inatumia Uchawi gan ktk maendeleo

ok buana waiter zungusha tena[emoji481] [emoji481] [emoji481] [emoji481]
 
Hilo taifa Mganga wao sijui ni Nan

au serikali yao inatumia Uchawi gan ktk maendeleo

ok buana waiter zungusha tena[emoji481] [emoji481] [emoji481] [emoji481]
taifa la marekani liliinuka na kuja juu kimaendeleo baada ya vita vya pili vya dunia baada ya kuamua kua nchi isiyofungamana na upande wowote (a neutral state), kwani nchi zilizokua juu kimaendeleo kama uingereza na ujerumani ziliathiriwa na vita hivyo. na hapo ndipo marekani ilipotumia mwanya huo kuzisaidia na kuzikopesha nchi zilizoathiriwa na vita, na hatimae marekani ikazidi kujiimalisha katika kila nyanja mpaka Leo unaiona Hapo ilipo.
note; marekani pia ilipitia changamoto nyingi sana ikiwemo za kiuchumi, kijamii na kiuongozi mpaka kufika hapo ilipo, UKIMUONA NYANI MZEE UJUE KAKWEPA MISHALE MINGI SANA.
 
Na wimbo wao wa Taifa "The Star-Spangled Banner" ulikuwa ni wimbo wa walevi katika vilabu vya pombe.
 
Hilo taifa Mganga wao sijui ni Nan

au serikali yao inatumia Uchawi gan ktk maendeleo

ok buana waiter zungusha tena[emoji481] [emoji481] [emoji481] [emoji481]
hata mimi sijui kwa kweli
 
maridadi kabisa hii
 
Lakini vita ya pili ilipigana na japani
 
Na ndio taifa lililowashikilia Waarabu middle East!! Wanahaha kila kukicha
 
ningependa kujua zaidi hapa mkuu
Mkuu nina haraka ila kwa kifupi........
The original song that used the melody was To Anacreon in Heaven, written sometime between 1760 and the late 1770s, expounding on the virtues of wine. The song itself was first publicly published in The Vocal Magazine in 1778 in London. The music was composed by John Stafford Smith and the lyrics are thought to have been written by Ralph Tomlinson, president of the Anacreon Society, which was a popular gentleman’s club in London whose membership were dedicated to “wit, harmony, and the god of wine”.
 
Mi ningependa kujua state zilizopo us pamoja na majiji mahalufu kwa kila state
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…