G-Mdadisi
Senior Member
- Feb 15, 2018
- 165
- 100
UKITAJA BIASHARA YA UTUMWA Duniani unaitaja Zanzibar #Unguja ambayo ndicho kilikuwa kitovu na soko kuu la Biashara hiyo ambapo watumwa walikusanywa kutoka pande mbalimbali Afrika (Kongo, Burundi, Rwanda, Tabora, nk.) kupitia Bagamoyo na kuletwa hapa kwaajili ya kuuzwa kwenda kutumikishwa.
PICHA 1&2: Ni kumbukumbu ya namna ambavyo watumwa walifungwa wakati wanasafirishwa, ambapo mpaka leo ukifika hapa utakuta kuna mabaki ya minyororo iliyotumika kuwafunga watumwa wakati wanasafirishwa kuletwa hapa.
PICHA 3: Ni Kanisa la Anglican ambalo lilijengwa na mumisioñari, Edward STEERE mnamo mwaka 1877 kwenye eneo ambalo biashara hiyo ilikuwa inafanyika ambapo lilijengwa baada ya kukomeshwa kwa biashara ya Utumwa, Edward Steere kwa kushirikiana na wamisionari wenzake akiwemo Dkt. LivingStone waliamua kujenga kanisa hili hapa kama sehemu ya kuzuia biashara hiyo na kukuza imani ya kikristu.
Tarehe 25,12,1877 kwenye sikukuu ya krisimass ndiyo ilikuwa ibada ya kwanza kusali katika kanisa hili kuu ambapo wakati huo lilikuwa halijaezekwa na mwaka 1880 lilikamilika rasmi baada ya kuezekwa. Mpaka leo mwaka 2023 kanisa hili lina zaidi ya miaka 140.
PICHA MWISHO: Chumba ambacho watumwa walihifadhiwa hapa baada kufikishwa Z'bar kabla ya kupelekwa sokoni kuuzwa. Wakati wa biashara ya utumwa kulikuwa na vyumba 10 ambapo Chumba kimoja cha wanaume (chenye ukubwa usiozidi 10x10) na dirisha moja tu, kilihifadhi watumwa 50, huku cha wanawake kikihifadhi 75 (wanawake 50 na 25 watoto). Na hapo chini kwenye mfereji ndipo ilikuwa choo chao walipojisaidia na kusubiri maji yanayotiririka yapite kusafisha.
Soko la watumwa lilikuwa linafanyika mara mbili kwa wiki, hivyo watumwa wote walifika na kuhifadhiwa kwenye vyumba hivi na walitolewa humu siku ya mnada kuuzwa, wale waliobaki walirudishwa tena kusubiri siku nyingine.
Ukifika hapa Zanzibar Ngome Kongwe, Yapo mengi ya kujifunza kuhusu BIASHARA HARAMU YA UTUMWA ambayo iliacha maumivu makali kwa babu zetu.
Karibu #Zanzibar
Visit Zanzibar
#VisitZanzibar
[emoji328] #GMdadisi
View attachment 2561559View attachment 2561560