Habari mbaya kwake ni ile penati aliyopiga fainali ya world cup 94 marekani, dhidi ya brazil kwenye dimba la rose bowl, pasadena, california... Mbele ya mashabiki 90,000+ hivi (sina uhakika kama tupac alikuwa mmoja wao)
Mwamba baresi alikosa ya kwanza ye akaja kukosa ya mwisho na kuwaua waitaliano wenzie na kuwaacha brazil wakibeba kombe lao la 4, likiwa la kwanza kwa hili jipya baada ya brazil iliyoshindika ya kina mtaalamu pele kubeba lile jingine la jules rimet trophy mara 3.