Machache unayotakiwa kuyafahamu kuhusu kilimo cha miembe cha kisasa

Machache unayotakiwa kuyafahamu kuhusu kilimo cha miembe cha kisasa

Joined
Sep 25, 2018
Posts
27
Reaction score
20
Mara nyingi kutokana na namna ya maisha na katika kupambana na gharama za maisha watu wamekuwa wanahangaika kutafuta namna ya kuzungusha pesa zao hasa katika njia zenye matokeo yenye mrejesho wa haraka,ila ni wachache wanasahau kuhusu dhamana iliyopo katika kilimo cha matunda hasa embe.

A. Embe maarufu duniani na sokoni ni;
1. Apple mango hasa nchi za mashariki ya kati huko.

2. Kent inafuatia wengi wanaijua hii ila changamoto ni kupigwa na nzi wa matunda ila ni tamu na linavutia.

3. Tommy Atkins hapa unaweza ukahisi ni jina la mtu ila ni moja ya maembe maarufu sana duniani.

4. Alfonso ila hili sio kwa kibiashara sanaa japo ni embe tamu toka likiwa bichi wengi wanapenda sifa yake hii.

5. Red Indian kutokana na rangi yake nyekundu linawavutia wengi.
Note; Mara nyingi rangi za embe zinawachanganya watu hivyo njia rahisi ni kuangalia umbo na msimu mfano Red ni nyekundu ila mengine ni mekundu ila yamechanganyika na rangi zingne. Hapa ni aina ambazo hupatikana kwa kubebesha na hazina asili ya nyumbani au almaarufu kama ''EXOTIC'' Japo lengo ni kuelezea umaarufu na faida ya embe husika kuna aina za maembe ya kigeni kama Palma na keitt na white soffa japo si maarufu. Kwa hapa nyumbani kuna embe kama kamba,bolibo na dodo ni nzuri sana kwa wale wasiotaka vitu vya kigeni.

B. Changamoto za kilimo cha maembe haya ni masizi ukungu (sooty mould) na fruitflies au nzi wa matunda hasa wa kiafrika,huyu ndiye anaongoza kuweka hasara kwa wakulima wengi hasa wale commercial,ila kuna namna za kuepuka hizi hasara maana huyu nzi analeta hasara kwa 80% so unaweza pata picha kwa ufupi.

C. Embe aina zote zipo kwa sifa zake na zinafaa kwa lengo lake yaani kuna nzuri kwa matumizi ya nyumbani hasa kwa juice,kuna zile ambazo zinachelewa kuvunwa na kuna zinazowahi,kuna zile ambazo zina uwezo wa kukinzana na magonjwa hivyo gharama za uendeshaji utapata picha kwa aina ya embe utakayochagua.

D. Embe ni moja ya matunda yenye faida kiafya na hata kibiashara,ni wewe na malengo yako tu kuhamua kufikisha kule kilimo uinataka kikufikshe.

karibuni kwa ushauri na huduma za miche ya matunda, mbogamboga na tiba.
simu namba; whatsup na simu 0714600575/simu na sms0620598113 au instagram @SHAMBA_INITIATIVES_OFFICIAL
karibuni sana tupo SUA PAROKIA YA MT. MARIA CONSOLATA.

20191218_164949.jpg
20191230_110746.jpg
20191230_111611.jpg
IMG-20191009-WA0015.jpg
 
. Changamoto za kilimo cha maembe haya ni masizi ukungu (sooty mould) na fruitflies au nzi wa matunda hasa wa kiafrika,huyu ndiye anaongoza kuweka hasara kwa wakulima wengi hasa wale commercial,ila kuna namna za kuepuka hizi hasara maana huyu nzi analeta hasara kwa 80% so unaweza pata picha kwa ufupi.
Matibabu yake ni yapi. Thi is the most importnt part.. Uchunguzi wangu mkoani tanga mjini ni kuwa miembe ya kisasa haizai kabisa! Ukungu na inzi ni wengi sana kenye embe ndani (wadudu ndani ya embe). Miembe inastawi lkn haizai, ikizaa ni embe mbili tatu .. or so
 
Apple mango yanachukua muda gani kuanzia kupandwa Hadi kuanza kuvuna?
miaka miwili na nusu hadi mitatu ila kukomaa au MATURITY ni miaka mi5,hivyo kuanzia miaka miwili na nusu utavuna ila ukikomaa utaenjoy sana kuanzia huo mwaka wa 5 utavuna sana sana
 
Matibabu yake ni yapi. Thi is the most importnt part.. Uchunguzi wangu mkoani tanga mjini ni kuwa miembe ya kisasa haizai kabisa! Ukungu na inzi ni wengi sana kenye embe ndani (wadudu ndani ya embe). Miembe inastawi lkn haizai, ikizaa ni embe mbili tatu .. or so
 
Matibabu yake ni yapi. Thi is the most importnt part.. Uchunguzi wangu mkoani tanga mjini ni kuwa miembe ya kisasa haizai kabisa! Ukungu na inzi ni wengi sana kenye embe ndani (wadudu ndani ya embe). Miembe inastawi lkn haizai, ikizaa ni embe mbili tatu .. or so
Hapo kwa fruit flies ni mitego tu ambayo ina pheromones kuzuia madume hivyo idadi ya uzaaji hupungua na kwa sootmould chanzo ni wadudu wafyonzao katika majani kama Aphids hivyo viuatirifu vyenye sumukiambato kama imidacropid zinafaa sana kupoteza hao wadudu na hivyo kupoteza madhara ya ufyonzaji wao ambao huleta weusi ambao huchangia kushuka kwa utengenezaji wa chakula kwa mmea (PHOTOSYNTHESIS)
 
asan te basi nipe specifically dawa gani ninunue please.
 
asan te basi nipe specifically dawa gani ninunue please.
Madawa yako mengi nadhani hapo ulipo kuna wataalamu sio wauzaji wa pembejeo watakuelezea ila jaribu kutafuta Confidor na zile za wadudu zenye viambato sumu zaidi ya kimoja.
 
Back
Top Bottom