Boeing 747
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 3,515
- 9,415
Mwanadamu huzaliwa, huishi kisha hufa. Sababu za kifo zinaweza kuwa kadha wa kadha mfano ugonjwa, kupigwa au ajali.
Linapokuja suala la ajali za barabarani, kuna sura tofauti tofauti kama vile waenda kwa miguu kugongwa na gari, gari kuanguka au magari kugongana..
Hivi juzi kati imeshuhudiwa kijana mdogo akipoteza maisha na kuicha familia yake ikiwa bado changa kabisa.
Moja kwa moja nijikite kwenye mada, sisi kama vijana tunaondesha magari kila siku, tufanye nini ili kupinguza ajali zinazofupisha maisha yetu na kuacha familia zinateseka. Inawezekana mada kama hii imeshawahi kujadiliwa, lakini si vibaya tukikumbushana tena kwa sababu vijana ndiyo tumekuwa wahanga wakubwa.
1. Kabla ya kuanza safari tuhakikishe vyombo vyetu vimekaguliwa kikamilifu na kufanyiwa marekebisho ya sehemu muhimu kama vile mifumo ya breki.
2. Kuwa na mpango mkakati kuhusu safari yako.
Panga muda wa kuanza safari, na kadiria muda wa kufika uendako.
Hii itakusaidia kuamua uendeshe kwa speed kiasi gani, wapi utapumzika.
3. Kumbuka uzoefu wa kuendesha mjini haufanani na uzoefu wa kuendesha highway.
Madereva wengi wana uzoefu wa miaka zaidi ya hata mitano kuendesha mjini, madereva hao hao wanapopata safari za mbali wanafikiria changamoto za mjini na high way zinafanana.
Kwa mfano, kuendesha kutoka Kimara mpka Posta kwa miaka sita, hakuwezi kufanana na kuendesha gari kutoka let say Ubungo mpaka Arusha kwa siku moja. Safari ya mbali inachosha na unaweza kusinzia hivyo ni vyema muwe angalau wawili kama ni mara yako ya kwana kundesha high way kwa muda mrefu.
4. Kumbuka kila dereva aliyepo barabarani ana safari yake.
Tuache zile ligi za kuona mtu amekupita basi na wewe unaaza kufukuzana naye..elewa aliyekupita humjui, hujui katoka wapi wala hujui anawahi wapi, huwezi kujua kalewa au anawahisha mgonjwa...hivyo baki kwenye speed uliyojipangia.
5. Epuka ku over take magari marefu kama malori kwa kukadiria endapo kuna gari linakuja upande wako. Hii imesababisha vifo vingi vya kugongana uso kwa uso.
Tuwe na tabia ya kujiridhisha kuwa ni salama kabla ya kulipita gari lingine..
6. Tuheshimu vibao vyote vya usalama barabarani...ikumbukwe walioviweka wana maana kubwa na walikuwa na upeo mkubwa pengine kuliko hata sisi
7. Siku zote chukulia kwamba dereva aliyopo mbele yako au nyuma yako ni kichaa..
Hii ina maana kwamba usimwamini dereva wa mbele yako au nyuma yako kwa sababu muda wowote anaweza kufanya maamuzi yanayoweza kukupelekea ajali.
8. Unapohisi kuchoka sana au usingizi usilazimishe kuendesha...kama una msaidizi mpe aendeshe au tafuta sehemu salama upumzike ikiwezekana ulale japo robo saa. Usingizi wa robo saa unaweza kukupa nguvu mpya kuendesha kwa masaa mengine zaidi ya matano.
9.Kama unatumia kilevi, epuka uwapo safarini, pia epuka milo yenye mafuta mengi uwapo safarini.
10. Usipuuze ishara yoyte ambayo ni ngeni barabarani..kuna wengine wanaweza kuona vitawi vya miti wakavipuuza, kumbe mbele kuna lori limeharibika. Hii imesababisha vifo vingi sana kwa kugonga malori kwa nyuma hasa nyakati za usiku.
Madereva wengi wa mjini wanaweza wasielewe hili. High way ina mambo mengi.
11. Uwapo high way jenga tabia ya kukaa angala mita 50 kutoka gari lililopo mbele yako...Hii itakusaidia kupata nafasi ya kujitetea endapo dereva wa mbele yako atafunga breki za ghafla.
12. Chukua tahadhari ya upepo mkali barabarani haswa kama unaendesha gari dogo sana..Kwa mfano, kuna eneo flani Same kama unatoka Dar kuja Moshi au Arusha, eneo hili lina upepo mkali unaoweza kulihamisha gari dogo kama passo endapo utaendesha above 80 kph..
13. Epuka mwendo mkali kwenye barabara ambayo ndiyo unaipita kwa mara ya kwanza, kwa sababu huwezi kujua baada ya mita chache kuna nini. Pia kuwa makini endapo hujapita barabara fulani kwa zaidi ya wiki moja, tunafahamu miundo mbinu yetu ni mibovu......leo lami ipo poa wiki ijayo ina shimo.
14.Tuache ile tabia ya kununua gari na kusema ninaenda kulitoa carbon.....wengi wamekufa wakidhani wanalitoa gari carbon, kumbe gari ndiyo linatoa roho zao.
15. Mwisho kabisa, kumbuka kuna watu wengi sana nyuma yako wanaokutegemea familia,ndugu,jamaa na marafiki.
**"*Tukizingatia haya machache, nina imani tunaweza kupunguza vifo vya ajali au ulemavu wa kudumu....vijana wengi ndiyo tumekuwa wahanga wa ajali za private cars na kuacha familia bado changa, au kuwaacha wazazi hawajaonja hata fadhila za kutuzaa na kutusomesha......sabau kuu imekuwa ni kutokuwa makini barabarani, mwendo kasi na ulevi.****
###### Kifo ni mpango wa Mungu lakini tusikilazimishe kwa uzembe####