ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 631
- 1,577
Changamoto ya upatikanaji wa mafuta na athari za matumizi yake ilipaswa kutumika kama sababu msukumo kwa Serikali kuongeza kasi katika kuhakikka taifa letu kutumika Nishati mbadala ambayo inapatikana nchini. Lakini tunaona kuna changamoto kuu mbili (2) kubwa; moja ni gharama kubwa za mfumo wa kutumia gesi na uhaba wa vituo vya kujazia gesi, licha ya hamasa kubwa waliopata watumiaji wa magari binafsi na waendesha bajaji kuhamia kwenye mfumo.
Katika bajeti ya wizara imeweka bajeti ndogo sana katika kuhakikisha taifa linahamia kwenye matumizi ya Gesi Asilia. Hotuba ya Waziri imeonyesha kwamba TPDC na GPSA ndio zipo kwenye hatua za awali za kufunga mifumo kwenye bohari za Serikali. Vile vile kuna karakana nane (8) za Serikali na binafsi zilizojengwa kwa ajili ya kubadilisha mfumo wa magari kutumia gesi asilia. Karakana zipo Dar es Salaam pekee.
Hatua hizi zinaenda polepole sana ukilinganisha na uhitaji uliopo. Waziri ameliambia Bunge kuwa vituo vya kujazia gesi asilia ni vipo viwili tu kwa Mkoa mzima wa Dar es Salaam. Kituo kinachomilikiwa na kampuni ya Dangote kilichopo Mwanambaya Mkuranga na kituo cha kampuni ya TAQA-Dalbit kilichopo pembezoni mwa barabara ya Nyerere karibu na Kiwanja cha Ndege (Terminal II) hata hivyo tunazo taarifa kuwa kipo kituo kingine kidogo maeneo ya Vetenari.
ACT Wazalendo, hasa kwa kuzingatia mizozo inayoendelea katika nchi ya Israel na Iran na nchi za mashariki ya kati na vita Ukrain na Urusi, tunaitaka Serikali
Mosi, Iweke msisitizo kwa TPDC na GPSA kufunga mifumo ya kuweka gesi kwenye gari za serikali haraka na gari zote za Serikali zifungwe mifumo hiyo.
Pili, Serikali iweke mazingira wezeshi kwa wauzaji wa maguta wa rejareja kuwa na Pampu za gesi asilia (CNG) kwa ajili ya kutoa huduma zote na kuweka vivutio kwa wawekezaji wa ndani kuwekeza katika utoaji wa huduma hiyo.
Tatu, Tunawasihi wasafirishaji wa Mabasi na malori ya Mizigo kufunga mifumo ya Gesi asilia katika vyombo vyao.
Nne, Serikali kupitia Naibu Waziri Mkuu ambae pia ni waziri wa Nishati kwa kushirikiana na Waziri wa Ujenzi kufanya tathmini ya gharama za ufungaji wa mifumo hiyo kwa vyombo vya usafiri kama gari ndogo na bajaji ili kuona namna ya kupunguza gharama ya kufungiwa mfumo huo.
Waziri Kivuli wa Nishati
Mwl Macheyeki Jr.
#10MaslahiYaWote
#10MamlakaKamili