ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 631
- 1,577
Kwa miaka mitatu ya bajeti kuanzia 2021 hadi 2024 pamekuwepo na tatizo la kupanda kwa gharama za mafuta ya Nishati (Petroli, Diseli na mafuta ya taa). Vile vile, robo ya pili ya mwaka fedha unaoishia Juni, 2024 tuliona kuongezeka kwa changamoto ya upatikanaji wa mafuta (uhaba wa mafuta). Tatizo la upatikanaji wa mafuta na gharama zake linahitaji hatua za makusudi za Serikali kuliko kusubiri sababu za nje.
Mwaka 2022/23 Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) amefanya ukaguzi wa Ufanisi kwenye eneo la usimamizi wa uagizaji wa mafuta nchini. CAG ameonesha kuwa nchi yetu haina hifadhi ya kimkakati ya mafuta ya Petroli kiasi cha kutishia usalama wa nchi. Aidha, CAG ameonyesha kuanzia mwaka 2020 hadi 2023 zinaonesha kuwa kampuni za uangizaji wa mafuta hazikuhifadhi mafuta ya kuweza kutumika kwa siku 15 wakati wote kati ya asilimia 12 hadi 62, na asilimia 14 hadi 65 kwa petroli na dizeli mtawalia.
Hii ni kutokana na Uzembe wa EWURA kufuatilia na kutathimini uwezo wa kampuni hizo badala yake ilikuwa inafanya makadirio ya jumla tu. Hivyo kupunguza uwezo wa kutambua kampuni ambazo hazikuhifadhi mafuta yanayotakiwa. Vilevile, CAG ameonyesha kukosekana kwa ripoti ya ukubwa wa soko kwa kila kampuni na kwa kila bidhaa kulipunguza uwezo wake wa kubaini hatari kwenye uhakika wa ugavi wa mafuta.
Jambo, jingine lililoonyeshwa na CAG ni uwezo mdogo wa miundombinu ya usambazaji wa mafuta. Anasema kwamba bomba moja tu linalotumika kuingiza mafuta Tanga, Mtwara na Dar es salaam na Bomba hilo moja ndio hutumika kusafirisha Petroli na Dizeli. Kiasi baada ya kusafirisha petrol linasafishwa ili kupitishwa Dizeli hii imepelekea uchelewaji wa kupakua mafuta kutoka 66-68 na kuongeza gharama za uchelewaji kwa Dola za Kimarekani Milioni 26.93.
Ni wazi kuwa matokeo haya ya ukaguzi na hoja zingine zipelekea kupandisha bei zaidi na kuongeza kiwango cha uhaba zaidi nchini. Waziri mwenyewe anakiri kuwa mafuta katika soko la dunia yameshuka kwa wastani asilimia 7 wakati bei zilizotolewa na EWURA zikionyesha kupanda zaidi. Hata nchini Jirani Kenya na Uganda mafuta yameonekana kushuka.
ACT Wazalendo tunataka Serikali ijenge uwezo wa Miundombinu ya kisasa na usimamizi wa hifadhi ya Mafuta nchini, tuwe na angalau hifadhi ya mafuta kutumika kwa miezi mitatu ili kupanda kwa haraka kwa bei ya mafuta katika Soko la Dunia kusitutetereshe kwa haraka.
Pili, Serikali iboreshe Miundombinu ya kupokeana kusambazia Mafmuta nchini ikiwemo bomba la kisasa la mafuta.
Tatu, Serikali irejeshe ruzuku kwenye mfuta ya petroli na Diseli kwakuwa sababu zilizosababisha kuwekwa hazijaondoka
Aidha, ni wakati sasa Serikali kuweka msisitizo wa kupunguza matumizi ya mafuta ya Petroli na Diseli kwa kutumia nishati mbadala ya Gesi asilia. Hii inawezekana kwa kuchukua hatua kadhaa za haraka;
i. Magari yote ya Serikali yaanze kutumia Gesi asilia (CNG) na bohari zote za Serikali (GPSA) zifungwe mitambo ya kujazia gesi asilia (CNG)
ii. Vilevile, mabasi ya mwendokasi nayo yabadilishwe mfumo na yaanze kutumia gesi asilia.
iii. Pia, magari ya abiria ya mikoani (mabasi) yote yafungwe mfumo wa kutumia mitungi ya Gesi asilia (CNG), ili kupunguza kutumia fedha nyingi za kigeni kuagiza bidhaa za mafuta.
#10MaslahiYaWote
#10MamlakaKamili