Machi 21 ni siku ya Down Syndrome

Machi 21 ni siku ya Down Syndrome

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Down Syndrome ni tatizo la kijenetiki linalotokana na uwepo wa kromosomu za ziada katika vinasaba vya urithi (DNA) vya Binadamu.

Tatizo hili husababisha mwonekano tofauti wa uso, ulemavu wa kiakili na ucheleweshaji wa ukuaji. Pia, baadhi ya watoto huzaliwa wakiwa na masikio madogo, shingo fupi, ulimi uliochomoza pamoja na misuli dhaifu ya mwili.

down-syndrome-illustration.jpg


Kauli mbiu ya maadhimisho ya Mwaka huu inalenga kutoa wito kwa watu na mashirika wa kueneza uelewa wa tatizo hili na kutowanyanyapaa waathiriwa.

Watu wengi walio na changamoto ya Down huonesha mapungufu yao usoni pasipo uwepo wa kasoro nyingine kuu za kuzaliwa. Hata hivyo wanaweza kuwa na kasoro moja au zaidi ya kuzaliwa au matatizo mengine ya kiafya. Baadhi ya matatizo hayo ni;
  • Kupoteza uwezo wa kusikia
  • Kuziba kwa mfumo wa hewa wawapo usingizini.
  • Maambukizi ya sikio
  • Magonjwa ya macho
  • Kasoro za moyo zilizopo wakati wa kuzaliwa
Watoto wenye tatizo la Down huhitaji usaidizi au uangalifu zaidi shuleni kuliko watoto wengine ili kuwajengea uwezo mzuri katika kujifunza.
 
samahani hiyo ''autism'' ni nini kama hutajali
Kwa kiswahili wanaita "usonji" mtoto anakuwa kama vile anautindio wa ubongo ila sio utindio wa ubungo. Sijui hapo umenielewa? mm sio mtaalamu sana ila natumaini watakuja wataalamu kuelezea vizuri
 
Back
Top Bottom