Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Maadhimisho ya siku hii hulenga kukumbusha Jamii kuchukua hatua madhubuti za uhifadhi wa maji ili kukabiliana na shida ya Maji Duniani kote.
Pia huangazia umuhimu wa maji na kutoa wito wa usimamizi endelevu wa rasilimali na vyanzo vya maji safi.
Haya ni Maadhimisho ya 30 tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1993 yakiwa ndani ya kipengele cha 6 cha Ajenda ya mwaka 2030 ya Maendeleo Endelevu (SDG) inayosisitiza Upatikanaji wa Maji safi na Usafi Mazingira kwa wote (clean water and sanitation for all) ifikapo mwaka 2030.
Kwa sasa, ulimwengu uko katika hali mbaya sana kwenye kufikia matamanio ya Ajenda hii ya 6 ya SDG 2030.
Taarifa zinaonesha kwamba Serikali zinapaswa kuongeza nguvu walau mara 4 zaidi kuliko hali ilivyo sasa ili kufikia Lengo hili kwa wakati.
Kutofanya kazi katika muda wote wa mzunguko wa maji kunadhoofisha maendeleo katika masuala yote makubwa ya kimataifa, kuanzia afya hadi njaa, usawa wa kijinsia hadi kazi, elimu hadi viwanda, majanga hadi amani.
Hivyo, mabadiliko ya haraka yanahitajika na kila mtu anaweza kutekeleza jukumu lake. Kila hatua hata iwe ndogo jinsi gani, italeta mabadiliko.