Samedi Amba
JF-Expert Member
- Nov 13, 2018
- 227
- 178
Habari WanaJF,
Natumaini tumeanza siku vizuri. Hata kama kuna mambo hayaendi, shukuru hata kwa uhai. Mungu yupo atakupambania...
Bila kupoteza muda, ningependa kuwashirikisha wazo, na naomba feedback. Kama mfanyabiashara, siku zote unatafuta pa kununua vitu kwa bei ndogo ili uweze kuuza kwa faida inayoeleweka.
Huenda unatafuta machimbo ya bidhaa za biashara.
Nimejikaza nikakusanya zaidi ya machimbo 300 Kariakoo ambapo unaweza kununua vitu kwa bei nafuu. (natazamia kufikia 1000+ hadi mwisho wa mwezi huu).
Sasa, nikaamua kutengeneza mfumo mdogo ambao utakusaidia kwa njia hii hapa:
Pamoja sana,
Amba Jnr.

- Utaingia kwenye mfumo (tutatumia web kwa sasa, apps zitakuja baadaye)
- Utachagua biashara unazotaka. Kwa mfano, sandals za kike.
- Utapata orodha ya machimbo, ila information utakayoona itakuwa ni jina na location ya biashara.
- Utachagua machimbo unayotaka kwa kuclick.
- Utapewa bei jumlishi ya machimbo yote ulochagua. (kila chimbo kitakuwa na bei
- Utalipia kwa njia unayopenda. Ama kwa simu au credit card (crypto baadaye).
- Utatumiwa list ya machimbo kwa njia ya SMS (jina na namba za simu) au email (Majina ya biashara, namba za simu, na location ya biashara). Tutafanya mpango wa Whatsapp baadaye.
- Je, ni nini kinakosekana hapo juu? Unahisi unaweza kuhitaji details zipi za chimbo ambazo hazipo hapo juu?
- Kwa sasa, ili kupelekwa kwenye chimbo na mwamba hapo Kariakoo, utalipia 5,000. Kwenye mfumo kama huu, unaweza kutoa sh. ngapi kuelekezwa kwenye chimbo husika?
Pamoja sana,
Amba Jnr.