Machimbo ya mfalme Suleiman hayafui dafu mbele ya machimbo ya prof. Ahmed Muhidin

Machimbo ya mfalme Suleiman hayafui dafu mbele ya machimbo ya prof. Ahmed Muhidin

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MACHIMBO YA MFALME SULEIMAN HAYAFUI DAFU MBELE YA MACHIMBO YA PROF. AHMED MUHIDIN

#21
Auz said:
Hazina ya kumbukumbu aliyonayo nyumbani kwake, ana mpango wa kuiweka wazi kwa hadhira?

Sent using Jamii Forums mobile app
Auz,
Mtu kama Prof. Muhidin ni msomi wa ngazi ya kilele na hapana shaka anajua umuhimu wa kuhifadhi ''machimbo,'' kama haya.

Hawezi kukubali kuyaacha yapotee.

Fikiria mtu nyumbani kwake ana friji inafanyakazi 24/7 ndani yake kahifadhi mikanda ya hotuba za Mwalimu kuanzia 1954.

Hizi ni hotuba za kudai uhuru.

Hotuba hizi ni zile alizokuwa akitoa Mnazi Mmoja.

Prof. Muhidin kanieleza vipi aliweza kufunguliwa hazina ya Baba wa Taifa na yeye wala si Mtanzania anaingia ndani ya chumba kile akawa anachukua na wakati mwingine kukomba kila alichokitaka tena ananambia kwa msaada wa Mwalimu mwenyewe.

Usuhuba huu kati ya Prof. Muhidin na Nyerere haukuwa wa kawaida.

Hawa walikuwa, "Two of a Kind."

Turejee kwenye mikanda yenye sauti ya Mwalimu wakati huo akizungumza Kiswahili kwa lafidhi ya Kizanaki.

Haya kanieleza Prof. Muhidin huku akicheka kwa kuwa anajua mimi ni Mswahili khalis na anaelewa Waswahili huwaje tunaposikia mtu anakizungumza Kiswahili vingine.

Hii ni mikanda ya ''reel to reel,'' na mingine ni cassette.

Chukulia kwanza kuwa dunia hii leo hakuna ''reel to reel tape deck,'' kama vile hakuna leo ''gramophone.''

Chukulia kwanza kuwa dunia hii leo hakuna ''reel to reel tape deck,'' kama vile hakuna leo ''gramophone.''

Leo utahangaika sana kuipata ''cassette player.''

Yeye Prof. Muhidin vyombo hivi anavyo.

Haya ya kwanza.

Hili la kutupia jicho naamini ikiwa mtu anataka kuangalia ''Machimbo ya Prof. Muhidin.'' kama nilivyofanya mie kisha akashika hamsini zake au ni kutafiti kwa muda mrefu bila shaka atamfungulia maktaba yake.

Msomi habanii elimu.

Mimi kanionyesha hadi chumba changu nitakachokaa ikiwa Insha Allah nitataka kwenda kufanya utafiti.

Prof. Muhidin ni msomi makini sana.

Nafikiria kuandika kitabu nikiite "Machimbo ya Prof. Taji Ahmed Muhidin."

Naamini sote tunakijua kitabu cha H. Rider Haggard, "Machimbo ya Mfalme Suleiman," (1885).

Rider Haggard alikuwa akiwaduwaza Wazungu wenzake wa karne ya 19 waliokuwa hawajui Afrika ilivyo kwa ngano za kusisimua na kutisha za Waafrika wanaoishi porini na watawala katili kama Twala na jicho lake la chongo na bibi kizee wake mchawi Gagula aliyemsaidia kuendesha serikali yake ya kidhalimu.

Prof. Muhidin nitamueleza katika Afrika inayojulikana ulimwenguni yeye akiwa kijana wa Mombasa aliyesoma Uingereza enzi za ukoloni na akaja kusomesha Chuo Cha Makerere chuo alichosoma utotoni na akasomesha na Canada.

Hakuna uchawi hapo wala ngano za kutisha hapo ni elimu pevu juu ya elimu pevu ndani ya bongo za vijana waliotaka kulikomboa bara lao la Afrika na wakimwangalia Julius Nyerere kama mfano wa kuigwa katika viongozi wa Afrika.
PROF. MUHIDIN NA PICHA ZA NYERERE.jpg
 
Nzuri Sana

Ndiyo imeishia hapa au kunamuendelezo?
 
Nzuri Sana

Ndiyo imeishia hapa au kunamuendelezo?
Mzee Mohamed heshima yako leo naomba niulize swali, hivi asili yako wewe haswa ni wapi!? maana kila kwenye andiko lako aghalabu uzungumzia lafidhi ya awali ya Mwalim.

Pia unajitabaisha kuwa wewe ni mswahili lakini hata waswahili wenyewe wana lahaja zao kulingana na wapi wanatoka na wala hawafanani: Kulikoni kushangaa lafidhi ya mtu? Maana asilimia 90 ya Watanzania ni watu wa bara! hata hawa vijana wa juzi wanaojiita watoto wa mjini asili yao ni bara! Sasa wewe asili yako ni wapi hali ionekane watu wa Dar es Salaam ndio wenye umuhimu wa pekee nchi hii?
Wabillah Tawfiq
 
Mwalimu Nyerere kuonekana kila pahali.
Kwa hakika Mwalimu alikuwa Mtu wa kipekee

Sent using Jamii Forums mobile app
Platozoom,
Alikuja Prof. mmoja kuzungumza na mimi kuhusu Mwalimu.

Tulifanya "session," tatu na yeye alikuwa kapita kwingi Ulaya na Afrika akiwahoji watu waliokuwa wana uhusiano na Mwalimu.

Mimi sikuwa na uhusiano wowote na Mwalimu ila nilikuwa nimemfahamu kupitia watu aliokuwanao kwa karibu wakati wa kudai uhuru.

Huyu Prof. akaniambia kuwa mimi nimewashinda wote kwa kueleza mengi ya Mwalimu ambayo wengine hawakuyajua.

Nakumbuka Zentrum Moderner Orient Berlin nilifanya mhadhara ambao Mwalimu alikuwa ndani ya kila mahali katika yale ambayo ndiyo yaliyojenga haiba yake kama kiongozi lakini tofauti iliyokuwapo nilieleza na wale ambao walishiriki pamojanae.

Hadhira yangu nilikuja baadae kuelezwa kuwa walifadhaika kwa kuwa walitaabika kuona Mwalimu ana-"share space," na watu wengine ambao wao hawakupata kuwasikia wakitajwa katika historia ya maisha ya Mwalimu.

Walipata tabu nilipoeleza "drama," ya uchaguzi wa Abdul Sykes na Nyerere kugombea urais wa TAA Ukumbi wa Arnautoglo mwaka wa 1953.

Walipata tabu kusikia kuwa kulikuwa na watu waki-"bank roll," harakati za uhuru hata hawajakutana na Nyerere.

Hawa wote na mchango wao kabla na baada ya kuungana na Mwalimu kwa hii hadhira yangu kwao kilikuwa kitu kipya.
Inataka ujuzi maalum wa historia ya Tanganyika kuweza kuchangia mjadala mfano wa huu kwa uhakika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee Mohamed heshima yako leo naomba niulize swali, hivi asili yako wewe haswa ni wapi!?maana kila kwenye andiko lako aghalabu uzungumzia lafidhi ya awali ya Mwalim,Pia unajitabaisha kuwa wewe ni mswahili lakini hata waswahili wenyewe wana lahaja zao kulingana na wapi wanatoka na wala hawafanani:Kulikoni kushangaa lafidhi ya mtu?Maana asilimia 90 ya Watanzania ni watu wa bara!hata hawa vijana wa juzi wanaojiita watoto wa mjini asili yao ni bara!Sasa wewe asili yako ni wapi hali ionekane watu wa Dar es Salaam ndo wenye umuhimu wa pekee nchi hii?
Wabillah Tawfiq
Mtoto,
Mimi ni Mmanyema nimezaliwa Dar es Salaam.
Sijapata kuzungumzia lafidhi ya Nyerere wala sijashangazwa na lafidhi hiyo ya Mwalimu kwani sijapata kuisikia.

Aliyeeleza lafidhi ya Mwalimu ni Prof. Muhidin.

Kuhusu watu wa Dar es Salaam kuwa na umuhimu hili si jambo muhimu sana kwani bila ya wengine kutoka majimboni kuunga mkono umoja usingepatikana na uhuru ungechelewa sana.

Kulikuwa na akina Abdallah na Maulidi Kivuruga kutoka Tabora kuwataja wachache.

Ali Ponda na Hassan Suleiman kutoka Dodoma, Sheikh Rashid Sembe, Mohamed Kajembe na wenzake kutoka Tanga, Paul Bomani na Saadan Abdul Kandoro, Ali Migeyo, Suedi Kagasheki kutoka Kanda ya Ziwa nk.
 
Mohamed Said, tuletee na habari za Hadija binti Kamba, mwanamke wa pili kuwa mwanachama wa TANU baada ya Titi Mohamed, nasikia yuko Ilala Bungoni anaumwa sana, ni vizuri ukaandika habari zake ubalance gender sijawah kuona ukizungumzia harakat za wanawake wa TANU kudai uhuru
 
Mohamed Said, tuletee na habari za Hadija binti Kamba, mwanamke wa pili kuwa mwanachama wa TANU baada ya Titi Mohamed, nasikia yuko Ilala Bungoni anaumwa sana, ni vizuri ukaandika habari zake ubalance gender sijawah kuona ukizungumzia harakat za wanawake wa TANU kudai uhuru
Laki...
Umekuwa unaniuliza maswali ambayo laiti ungesoma kitabu cha Abdul Sykes kama nilivyokuelekeza huko nyuma usingeuliza.

Wanawake nimewataja.

Kwanza Bi. Khadija fahamu ni marehemu na wala si mwanamke wa pili kujiunga na TANU.

Pili nimewataja akina mama wengi katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika:

Bi. Hawa bint Maftah, Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Zarula bint Abdulrahman, Bi. Chiku bint Said Kisusa, Lucy Lameck, Bi. Halima Selengia, Mama bint Maalim, Fatma bint Matola, Bi. Sharifa bint Mzee...

Narudia tena.

Soma kitabu cha Abdul Sykes kipo katika mzunguko toka mwaka wa 1998.

Angalia:

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI - TANZANIA: NANI ANAWAJUA WAPIGANIA UHURU HAWA WANAWAKE?

Soma taazia ya Bi. Khadija hapo chini:

TAAZIA: BI. KHADIJA BINT KAMBA (1922-2016) MWANAMAMA MPIGANIA UHURU - MAKALA HISANI YA SAIGON GROUP

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom