Machine za kutoa sumu mwilini

nimegundua...kumbe lishe bora ndo dawa jamani. tunda sana+maziwa sana
 
Njia kuu ya kuondoa sumu mwilini ni mboga mbichi mchanganyiko SALAD:

Hakikisha unapata mchanganyiko wa mboga mbichi zifuatazo:

Koliflawa kipande kidogo, mchicha kiasi, kabeji kidogo, mdalasini 1/4 kijiko kidogo, kitunguu maji kidogo, kitunguu saumu punje tatu, spinach kiasi nyanya moja itolewe mbegu si kiini chake na mboga zinginezo ukipenda unaweza kuongezea. safisha vizuri mboga hizo na uzikatekate weka chumvi 1/8 ya kijiko kidogo (cha chai) changanya chumvi hiyo mpaka ichanganyike vema na mboga zako. subiri kwa robo saa, kamulia limau au jamii yake na kisha kula.
Ni vema kula kachumbari hiyo kila baada ya mlo wako wa usiku. unaweza kunywa pia glasi ya maziwa moto yaliotiwa asali si sukari.
HAKIKISHA UNAPATA VITU HALISI.
Namaanisha mboga zisiwe na sumu au zilizorutubishwa.
 
Kiasili, dawa yenye kuondosha sumu za mwili kwa uhakika ni UKOKA, (ukoka ni aina ya nyasi zenye mizizi mirefu inayotambaa sana ardhini, mizizi yake huwa na pingili kama za miwa) watu wa mashariki ya mbali ndio wakitumia kwa ajili ya kuondoa sumu mwilini. hupondwa na kurowekwa kwenye maji kisha hunywewa. hakuna kipimo maalum! kunywa kadri unavyoweza!!

Watu wa mashariki ya kati hutumia mizizi ya mtende, hurowekwa kwenye maji mchana kutwa na usiku hunywewa.

Wengine hutumia kupiga chuku, aidha wengine hutumia sindano za kichina.
 
hapa kazi ipo kila mtu anatoa anachokijua, ila Yote ni kula vizuri, matunda kwa wingi, maji ya kutosha , kupumzika kwishnee
 
Mchanganyiko wa matunda (fruit salad) na maji kwa wingi ni kianzio kizuri tu
 
ukitaka kutoa takataka juu ya ngozi yako unafanyaje? unaoga kwa kutumia maji. ukitaka kuondoa uchafu kwenye nguo zako unatumia nini? utafuwa kwa kutumia maji. ukitaka kusafisha sakafu nyumba yako unafanyaje? utadeki ukitumia maji. MAJI pekee ndiyo dawa bora ya kuondoa sumu mwilini bora kuliko kitu kingine chochote duniani, watu kadhaa tayari wamekuambia utumie maji. unajuwa namna ya kunywa maji? bonyeza: Utangulizi | maajabu ya maji
 

Pole sana ndugu yangu. Virutubisho vya kuondoa sumu mwilini vipo.....nina mjomba wangu ametumia vimemsaidia sana. Alikuwa akisumbuliwa na kuwashwa na ngozi na malenge lenge. Ametumia for 3 weeks yuko fine. Uzuri wake ni kwamba virutubisho hivyo vinatambulika kimataifa na kufanyiwa uchunguzi wa miaka 25. Vimezibitishwa na baraza la scientists Israel na marekani....ukizingatia unapewa gurantee ya mwezi mzima. Kama hujaridhika navyo unarudishiwa pesa yako.
 
zipo na tena nidawa ambazo vimetengenezwa kiasili kwa maelezo zaidi na kwa matibabu fika pale kurasini kupitia shimo la udongo kwenye ofis za wapo radio kuna hosp ya kanisa
 
Mjini shule. Mnatoka vijijini mnaingia mjini kichwa kichwa, lazima mpate darasa la nguvu!
 
Hii kitu nimeisikia sana...sijawahi kujaribu fuatilia maana niliona haiingii akilini. Pengine kuna technolojia bado haijawekwa wazi....na ni kwa namna gani watumiaji wananufaika nayo?
 
Hata mimi sijaelewa ni jinsi gani uchafu unatoka mwilini kwa speed kali namna hiyo! Labda waliojaribu watuambie vizuri
 
Swali la kujiuliza ni kwamba, hivi sumu za mwilini ni lazima ziwe na rangi? Sumu nyingi nijuazo hazina rangi na zinatambuliwa kwa kutest composition sio kwa macho!!
Nini kinathibitisha hizo ni sumu? Tupeni elimu!
 
vypte hivi ni sumu tu.
Haya soma hapa
(1) Tumia sana juisi ya rozella
(2) Tumia sana asali
(3) Tumia sana mdalasini
(4) Tumia sana kitunguu saumu kilichosangwa.

Nawasilisha.
 
Hata mkoa wa Kagera hao watu wapo na wanapata wateeja sana, Labda serikali ifuatlie kuhusu ukweli wa hizo sumu kutoka, lakini ni kweli ukiweka miguu kwenye karai la maji baada ya muda maji yanageuka rangi, na unaambiwa hiyo yote ni sumu toka mwilini mwako.
 
Mungu aliyetuumba alishaweka viungo ndani ya miili yetu vya kushughulika uchafu wa mwilini ikijumuisha figo, ini, ngozi n.k. Topic hii iko tangu shule ya msingi - excretion. Mwili unatoa uchafu kwa njia ya haja kubwa, mkojo, jasho na kadhalika. Labda kama kuna matatizo na viungo hivi! Watu wanaenda kulipa kutolewa uchafu!!! Mungu alishatupa mashine hizi bure!!! Topic hii ilishawahi kuja hapa JF na nikauliza hawa jamaa kwa nini sumu zao wanazotoa lazima ziwe na rangi? Kwa sababu ni lazima uone ile uwe convinced. Tafakari!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…