Machinga hatutaki ''Mamluki''

saidoo25

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
624
Reaction score
1,456
Mwenyekiti wa shirikisho la wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga Mkoa wa Mbeya Jerry Mwatebela amesema uchaguzi uliofanywa Ili kuwapata viongozi wa soko la airport ya zamani ni batili kutokana na kughubikwa na utata katika zoezi Zima la uchaguzi huo.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Mwatebela, amesema uchaguzi huo ulikua na makandokando mengi ikiwemo wasimamizi kuwaingiza watu kupiga kura baada ya muda wa uchaguzi kuisha, sambamba na kuwepo Kwa kura zilizo ibua shaka baada ya kukutwa zikiwa zimekunjwa pamoja katika makundi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa shirikisho hilo Wilaya ya Mbeya Waziri Hamisi, amesema baada ya kuwepo Kwa sintofahamu hiyo wao kama shirikisho waliamua kuitisha uchaguzi ulio simamiwa na shirikisho la wamachinga, na kuwezesha kupatikana viongozi wapya baada ya kufutwa uchaguzi wa awali.

Baraka Mwaihola ni mwenyekiti mpya wa soko hilo la machinga ameahidi kushirikiana na wafanyabiashara katika kuhakikisha wanashirikiana na Serikali Ili kuyafikia Maendeleo, wakati wamachinga wakiomba viongozi hao kuto ruhusu mamluki wenye maslahi yao kuingia katika uongozi wa soko.

Cc: wasafifm
Cc @enocksaimon
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…