Business is not for everyone.
Wafanyabiashara machinga wa makoroboi na langolango mmepoa sana, soko zima husikii kelele za kuita wateja wala zile spika za amsha amsha.
Utadhani uko supermarket, hata supermarket kuna music laini hupigwa.
Hakuna kubembeleza wala kumshawishi mteja, hakuna kusema karibu, unataka utanunua hutaki nenda.
Hali ni tofauti kwa wenzao wa Karume na mitaa ya Kariakoo. Kama ni mgeni utarudi kwenu na mawenge ya kelele usiku kucha.
Mmepoa, mmepoa.