Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 242
- 1,141
Wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga katika Soko la Simu2000, jijini Dar es Salaam wameanza mgomo asubuhi ya leo Jumatatu Julai 8, 2024 kwa kufunga barabara, huku wakiimba nyimbo za kudai haki yao.
Wamachinga hao wanadaiwa kulalamikia mpango wa sehemu ya eneo wanalofanyia kazi zao kukabidhiwa kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart).
Kwa mujibu wa wafanyabiashara hao, Dart inapewa eneo hilo kwa ajili ya kujenga karakana ya mabasi yake mbadala wa ile iliyopo Jangwani, jijini Dar es Salaam.
Kinachozusha hofu miongoni mwao ni kile wanachoeleza walikabidhiwa eneo hilo na kuahidiwa ndilo litakalokuwa rasmi kwa shughuli zao, baada ya kuhamishwa kutoka maeneo mbalimbali.
Sambamba na hayo, wamachinga hao wana hofu uwepo wa Dart katika eneo hilo, utawaondoa baadhi yao, pia kukiondoa Kituo cha Daladala cha Simu2000 ambacho ndicho tegemeo lao la kupata wateja wanaofika hapo kusubiri usafiri wa kwenda maeneo mbalimbali.
Mbali na kufunga biashara zao, pia wameweka vizuizi katika barabara kuelekea Sinza na kuzuia magari kuingia na kutoka katika kituo hicho cha daladala.
Nyimbo za 'hatutaki karakana, tunataka soko letu' ndizo zilizokuwa zikisikika zikiimbwa na waandamanaji katika eneo hilo.
Wafanyabiashara hao pia walikuwa na mabango yenye jumbe mbalimbali, ikiwemo 'hatutaki karakana Simu2000 Mama Samia njoo ututetee.'
Mwananchi
===
CHALAMILA AWATULIZA, HALI YA HEWA YATULIA YATULIA
Wafanyabiashara wadogo maarufu kama "Machinga" zaidi ya 500 eneo la Soko la Mawasiliano (SIMU 2000) wameandamana wakidai kuwa wamepokea taarifa inayowataka kupisha eneo waliopo kwa ajili ya ujenzi wa karakana ya Mabasi ya mabasi ya mwendokasi (UDART).
Wafanyabiashara hao wamedai kuwa hawaungi mkono suala hilo kwa sababu wamewekeza fedha zao kwa kujenga mabanda sambamba na miundombinu mingine ya kibiashara.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo alifika eneo wafanyabiashara hao hawakumpa ushirikiano, hivyo akalazimika kufika Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ambaye amesema kuwa kero hiyo wameipokea na kuwa siku ya jumamosi Julai 13, 2024 atarudi tena kutoa muafaka wa suala hilo na kuwataka kuendelea na biashara zao.
Pia soma: