kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Nimewasikia wafanyabiashara wa kariakoo wakipendekeza serikali iwarejeshe machinga vijijini wakalime. Nimewasikia wanasiasa wakiunga mkono hoja hii wakidai endapo vijana watajiajiri kwenye kilimo maisha yatakuwa mazuri kwao na familia zao.
Niliposikia kauli hizi nikajiuliza machinga ni wakina nani?Katika kutafuta majibu nikaelekeza fikra kwenye malango ya machangi kuingia kazini kwao. Lango la Kwanza nililoangazia ni kariakoo, hapa ntatoa mfano mmoja tu ambao mliopo Dar es salaam mnaweza Leo au kesho mkatuwekea hapa uthibitisho.
Damka asubuhi saa kumi na mbili nenda kituo Cha treni,dalafala na mwendokasi Cha gerezani. Angalia idadi ya vijana wanaoletwa mjini kutokea Mbagala, Gongo la Mboto na mbezi, Hawa ndio wanachinga. Ukiangalia wengi wao wana familia na Wana watoto wadogo. Tunaambiwa kirahisi kabisa na viongozi wa wanachinga na viongozi wa kisiasa kwamba Hawa watu Ni kero mjini hivyo wafanyiwe figisu warejee kijijini. Naamini viongozi na watu wanaowaza namna hii Wana matatizo ya akili.
Kundi hili linakwenda kuhatarisha usalama wa Raia mtaani, wanakwenda kuanzisha panya road na mkiwakamata mtaambiwa ninyi ndio mmewafukuza kwenye vipato vyao.
Nimuulize RC na timu yake, Hawa wanachinga waliwekwa barabarani na JPM na Hadi siku anafungua kituo chake Cha Mbezi tulimsikia akiwaita wakafanye biashara ndani ya kituo na wasibughudhiwe. Leo nani anaweza kutuonyesha kariakoo machinga wamehamishiw wapi? Mbezi Luis wametengewa eneo wapi? Gongo la Mboto na Chanika wapi pametengwa? Tegeta, boko na bunju je? Mbagala, Tandika na temeke? Huku kote hakuna maeneo wakauze Nini?
Lakini pia Jambo lakushangaza nikusikia Rukwa nao wanapambana na Machinga, Kigoma, Tabora, Mtwara, Lindi, Tanga, Shinyanga na Mikoa Kama hii nayo wanapambana na Machinga. Are we serious? Kwamba huku nako Kuna machinga? Kwamba Wakuu wa wilaya nje ya Dar na Mwanaza pamoja wakuu wa Mikoa nao Wana agenda ya machinga? Nadhani wakuu wa Mikoa mingine fanyeni kazi acheni kusumbua raia, Tabora tuseme wamekwama Hadi Rais? Rukwa? Moshi?
Badala ya machinga kurudi vijijini wanarudi mitaani na hapo ndipo mtajifunza Nini wafanyakazi, mkiibiwa mtajua kwanini ajira ni muhimu.