13 November 2021
MACHINGA WAVAMIA ENEO LA KANISA BAADA YA KUHAMISHWA, TAHARUKI KUBWA YAIBUKA
Mgogoro mkubwa umeibuka kati ya Kanisa la Orthodox lililopo Mbuyuni, Salasala jijini Dar es Salaam na wafanyabiashara ndogondogo wa eneo hilo maarufu kama wamachinga, ambapo uongozi wa kanisa hilo unadai kwamba eneo lao limevamiwa na wafanyabiashara hao na kujenga vibanda kiasi cha kusababisha washindwe kufanya ibada. Global TV imefika eneo la tukio nakuzungumza na pande zote mbili, ambapo upande wa wafanyabiashara hao, wanadai kwamba hilo ni eneo la wazi na kwamba hawajavamia eneo la kanisa, kauli ambazo zimeungwa mkono na viongozi wa serikali ya mtaa.
Source : Global TV online
Toka maktaba :
24 October 2021
MAKAMU wa RAIS DKT PHILIP MPANGO AKUTANA na BABA MTAKATIFU wa ORTHODOX AFRICA....
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango leo Oktoba 24,2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Baba Mtakatifu Beatitude Theodoros II (The Pope and Patriarch of Alexandria and all Africa)Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Greek Orthodox Ikulu Jijini Dar es salaam. Makamu wa Rais amesema Tanzania imefurahishwa na ujio wa Baba Mtakatifu huyo na kumuomba kuendelea kuiweka nchi ya Tanzania katika maombi yake ya kila siku. Amesema tangu kupata uhuru Tanzania imekua kitovu cha Amani na kuendelea kuheshimu umuhimu wa dini zote kupitia ibara ya 19 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha amesema viongozi wa dini nchini Tanzania wamekua ndio msingi wa Amani iliopo nchini. Makamu wa Rais ameongeza kwamba Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inatambua mchango mkubwa unaotolewa na taasisi za dini hapa nchini kwa kushirikiana vema na serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo husasani katika sekta za elimu na afya hasa katika maeneo ya pembezoni ya nchi. Ametaja mchango wa kanisa la Orthodox nchini ambao ni pamoja na ujenzi Kliniki 90 pamoja na Hospitali katika mkoa wa kagera na shule katika maeneo mbalimbali ya nchi.