A
Anonymous
Guest
Harufu ya machinjio iliyopo katika Manispaa ya Morogoro imekuwa kero kwa wakazi wanaozunguka eneo hilo pamoja na wapitanjia kutokana na miundombinu kuwa mibovu hasa ya kupitisha maji machafu.
Eneo hilo maji machafu yanayotoka katika machinjio hayo yamekuwa yakizagaa hovyo na kutuama mpaka kupelekea harufu inayowakera watu.
Kibaya zaidi maji hayo yanafika hadi kwenye mitaro ya barabara kipindi cha mvua hali ndo huwa inakuwa mbaya zaidi kwani hali hiyo inaweza kupelekea hata magojwa ya milipuko.
Mamlaka husika hasa Manispaa inatakiwa kuweka miundombinu rafiki ya kupitisha maji machafu yanayotoka katika machinjio hayo mfano mabomba ambayo yanaweza kupitisha maji yajengewe na chemba ili hayo maji yaweze kupita huko kama maji taka ili yasiyo yanazagaa au yasiwe kero kwa watu.
Mabomba ya maji taka nayo hayapo katika mfumo mzuri kuna muda mvua zikinyesha hali inakuwa mbaya kuliko maelezo kutokana na uchafu unavyosambaa.
Majengo ni chakavu
Sisi ni walaji tumekuwa na shaka juu ya ubora wa mboga inayopatikana eneo hilo upande wa afya, kwa ufupi linatakiwa kuwa na muonekano mzuri lakini uhalisia majengo ni chakavu na kiasi kwamba akitokea mgeni akafika hapo anaweza kuhisi yametelekezwa.
Sehemu za kuhifadhia taka napo kuna muda zinajaa licha ya kuwa kuna sehemu mbili, zinaweza kujaa na kumwagika huku shughuli ya uchinjaji ikiendelea kama kawaida.
MKURUGENZI AGOMA KUZUNGUMZA
JamiiForums ilipowasiliana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro, Emmanuel Mkongo kuhusu hali hiyo, amesema “Uje ofisini siwezi kuzungumza mambo hayo kwenye simu” kisha akakata simu, alipopigiwa baadaye hakupokea.