Wasanii wa hip hop wengi wana stress, nimeusikia wimbo lkn naona kama braza stamina kaishiwa mbona Jay moe kaflow vizuri, au anaona akitaja wcb ndio nyimbo itahit, mwanangu stamina unaendelea kufeli. Kinachowafelisha wasanii wengi wa hip hop ni kung'ang'ania nguzo, hizo nguzo za hip hop zimekuwa labda nguzo tano za kiislam au amri kumi ambazo zimewekwa na mungu hazibadiliki na hazitobadilika,
Culture is DYNAMIC na nyie wenyewe mnakiri hip hop ni utamaduni lkn bado mpo STATIC siku zote watu wanawachoka beat zile zile, flow zile zile mbona Joh makini, niki wa pili, warawara sijawasikia wakilalamika nashow wanapata, airtime wanakata ya kutosha. Hawajifunzi kwa moe tech na prof wamebadilika japo kuwa zamani walikuwa wanakaza kuliko wao, hebu angalia pesa ya madafu na kazi kazi zinavyopata air time, hii yote kwa sababu wamebadilika.
Nyie wenyewe mnakiri hip hop ni culture and always culture is DYNAMIC not STATIC sasa nyie mnakuwa against na hip hop kwani bado mpo STATIC na watu watachoka kuwasikiliza na mtaishia kuwachana diamond platnumz, wcb, weusi, babutale na fella ila wenzenu wanapiga ela tu, sasa sijui mkiwamaliza mtahamia kwa nani, badilikeni gem lipo fear mimi mwenyewe siku amini kama prof jay atafanya hip hop kwa mtindo wa singeli, Joh makini kufanya hip hop ktk beat za afro pop bado pesa ya madafu na sweat mangi zote hizi nyimbo kali na ukali wake umetokana ubunifu wa Hali ya juu, badilikeni.