Orketeemi
JF-Expert Member
- Feb 12, 2013
- 5,063
- 12,866
Wakuu nipo Dar na kwa kweli nimeshuhudia mengi ambayo kiukweli ni fursa kubwa ya kupata pesa.
Kwa mfano nimeshuhudia Dar viazi mviringo vitatu tu tena vya ukubwa wa kawaida kabisa vikiuzwa kwa shiling 500.
Sado moja la viazi mviringo likiuzwa hadi shilingo 4000. Hapa mtu ukiwa Mbeya ambapo gunia la viazi lenye debe 6 mpaka nane unaweza ukalinunua kwa shiling elfu 40-50 . Ushuru ni 500 kwa kila gunia na usafiri ni kati ya 7,000 -10,000 kwa gunia mpaka Dar.
Kama unachukua gunia 20 ina maana utagharamia 1,200,000 maximum mpaka mzingo unaingia sokoni. tufanye umeamua kujumlisha kwa elfu 75-85 kwa gunia maana yake unakusanya 1,5000,000 Mpaka 1,850,000 kwa mzigo wote. Hapo hukosi faida ya 300,000.
Kuna fursa nyingine ya mchele kutoka Mbeya ambapo mchele super kabisa nimeona ukiuzwa kwa kilo shilingi 2,700 wakati Mbeya mchele grade hiyo hiyo ni 32,000 -34,000 kwa kilo 20. Sasa tufanye unachukua mfuko wa kilo 100 kwa shiling 160,000 - 170,000.
Unachukua tani 1 tu za mchele ambapo ni kwa gharama ya 1,600,000 mpaka 1,700,000
Nauli kwa mfuko wa kilo 100 ni 7,000 mpaka Dar jumla unalipia elfu 70 tani moja. ushuru tufanye elfu 10 tani moja au elfu 20 pamoja na kupakia elfu 10 pia na kushusha 10. jumla.
Ukifika Dar utajumlisha kilo 20 kwa elfu 42 mpaka 44. kwa mfuko wote unapata 210,000 mpaka 220,000 una viroba kumi maana yake unapata 2,200,000 au 2,100,000. Ukitoa gharama zote unapata faida angalau 350,000 mpaka 400,000
Mwenye uzoefu na biashara hizi anisahihishe.