Macho yako yanaona kama mimi? Mimi naona kama DSM fursa za kupiga pesa ni nje nje

[emoji58][emoji58]Daaah hii inaleta ugumu sana kwa watu kuingia ktk hizi mishe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa kaleta fursa, watu wameleta kejeli tena 90% walioleta kejeli ndo wale wanaonzishaga thread za "NINA (KIASI FLAN) NIFANYE BIASHARA GANI?"
Hao wanao comment ndio wenye uzoefu baba usiongee kinadhalia,kwenye nyeusi tuseme nyeusi na nyeupe tuseme nyeupe hakuna kupepesa mambo,mfumo unamnufaisha dalali kuliko mkulima na mfanya biashara wa kati.
 
Wajuaji walishindwa ku concentrate na uzi,wakaaza kum dhihaki mtoa mada, mbona biashara hii kuna watu wanafanya!!.Ilitakiwa watu wafikirie challenges za hii business na namna ya ku tackle.Sasa mtu anakuja kuongelea vitu kama "uchawi",unajuaje labda na yeye anaamini katika "kujidhatiti".Issue ilikuwa ni kumpa changamoto za usambazaji/uuzaji na logistics nyinginezo
 
Changamoto ndio hzo na uchawi nao upo tena sana tu,wee ulitaka tumperembe perembe mleta uzi.Wakati tunasoma biashara vyuoni maprofessa walitufundisha tu biashara ila ukija field ndio unagudua kwamba hata professor wako aliyekufundisha biashara hakuwa mfanya biashara so kuna mengi hakukufundisha.
 
Sasa ulitaka nizungumzie wanawake wenye makalio makubwa?? Hata mtu wa Dar akienda mkoani ataziona fursa na kubaki kinywa waz
Mkoani fursa zipo ila hela sio nyingi kama Dar!

Changamoto iliopo ndio hio!
Kutengeneza laki 1 dar ni kwepesi kuliko kutengeneza pesa hio hio kwenye baadhi ya mikoa ila pia laki hio moja kutosheleza mahitaji yako mkoani ni kubwa sana tofauti na DSM.

Ukiweza kuwa stinji kwa Dar ni rahisi sana kufanya maendeleo maana ukusanyaji wa pesa nyingi ni rahisi tofauti na mkoani ambapo unakusanya slowly.
 
🤣🤣🤣🤣🤣 Usiombe ile moment umefika sokoni huna moja wala mbili za hio biashara kmmmae. Movie inaanza kila gunia linatakiwa lilipiwe 600 ya ushuru, kulaza gunia dagoni ni 200 kwa siku.

Nakumbuka niliagiza mzigo wa kitungu u toka Arusha. Niliemtuma hakukagua akavalishwa vitunguu gunia 6 chenga tupu. Mzigo ukawa unanitesa kwanza ulfungwa kwenye viroba ikabidi kuufaulisha kwenye magunia. Hapo sijaingiza hata 100 mzigo mara ukaanza kuota ndani ya gunia joto la dar. Aisee nilijuta.

Nilishuhudia laki 8 yangu inapukutika kama maji pale sterio! Stress niliokuwa nayo ilinibidi niwe nadamka saa 10 kwenda kumwaga mzigo mezani aisee nipambanie kuuza kitunguu kelele mingi kama konda. Bahati nilikuwa na Aunt yangu pale sokoni akawa ananipa emotional support. Nilichofanikiwa kuokoa ni 110,000 na gunia moja na nusu. Kilichotokea na hio hela nayo ilipotea.
 
Mkuu Mkaruka

Jamaa yako ilitakiwa atumie mbinu za kijasusi, angeenda Moro akanunua mbuzi wanne then akaenda nao pugu (hao mbuzi ni sample ya kupata detail jinsi biashara inavyofanyika) then akajifanya anawauza (hapo ni Aidha apate faida au loss), angeusoma vizuri mchezo kama ni mjanja angepata na connection kabisa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu tusome mada mpaka mwisho. hakuna kisicho na changamoto ndio maana nimesema mwenye uzoefu anisahihishe.
kuna jamaa wanaitwa madalali...

kuna low demand na high supply kiazi hakina uvumilivu
 
Mtu mwenye mihemko ya kichuo hawezi kuwa na akili hiyo Mkuu.

Ukiwa chuo unaona kama mtaani kote kumejaa wajinga, hawaoni hizo fursa.
 
hukutaka mzigo wako kutuachia sisi madalali
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hapo ndo akajifunza nn maana ya subira ..papara mbaya Sana

One love
 
Nimesoma hii mada na kupitia comments za watu, mbali na kujifunza mambo mengi pia nimecheka sana. Full burudani.

Kweli biashara sio hesabu ya 1+1=2 bali biashara ni 2+x-y=z÷3.
 
Kuna wakati huwa nahisi mtu kuweza kufanya biashara fulani basi inabidi uwe na hicho kipaji.
 
Kwenye research kuna kitu kinaitwa Research Problem nia kubwa ya Research problem ni kujaribu kuangalia ni vitu gani ama matatizo gani yanaleta changamoto mpaka Research ihitajike sasa basi ni bora kuanisha changamoto ni zipi na njia ya kupambana nazo.
 
Wazo ni kitu muhimu sana kwenye biashara unafikiri mtu aliyeandaa project ya azam juice ya ukwaju hakujua zile ups and down hebu tufikiri tofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…