Macho yako yanaona kama mimi? Mimi naona kama DSM fursa za kupiga pesa ni nje nje

Aisee! mwezi ulopita nlipeleka mitumba yangu mnadani siku ya kwanza niliuza balaa nikasema biashara c ndo hii, sasa minada ilofuatia ilikua kuipata elf 30 ni ndoto ya alinacha, kuna mdada akanitonya huku kuna ushirikina balaa we umekujaje? Looh nikaamua nibebe mizigo yangu kuirudisha nyumbani hapa naumiza kichwa pa kuipeleka!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cha ajabu huku wanaotufundisha hizo research hawajawahi kufanya application yake huku mtaani zaidi ya wao kukariri tu.
 
Bila shaka utakuwa milionea
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Huwezi mkwepa dalali mkuu...wana techniques kama zote
 
Ukiwasikiliza watu wa jf hakuna biashara yoyote utakayofanya hapa duniani maana kila biashara wanaikandia ila ukweli ni kwamba hakuna shughuli yoyote ya kiuchumi isiyo na changamoto,Cha msingi ni kukaa chini na kutafakari namna ya kukabiliana na changamoto hizo,Mimi ningekushauri Kama unataka kufanya hii biashara Kodi fremu ukitoa mazao yako mikoani uwe unafikishia hapo Kisha uwe unawauzia watu mitaani yani unapita nyumba kwa nyumba kuliko kupeleka kwenye masoko maana huko Kuna madalali watakulalia sana.
 
Hebu jaribu kiongozi halafu ulete mrejesho hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezi mkwepa dalali mkuu...wana techniques kama zote
Basi Niko mgeni kwenye biashara ya ng'ombe,nikasema nianze na ng'ombe mmoja tu,nikila hasara sirudi.
Basi nikanunua ng'ombe mmoja mdogomdogo wanaita kadogosa,,maana ya haraka haraka Ni ng'ombe mbinti hajazaa,
Nikanunua 250,000,
Baada ya Hapo unakabidhi mswagaji,,unakua huamini amini maana unampa bila documents zozote,lakini Hawa waswagaji Ni waamunifu Sana,
Nikamwambia peleka mnada fulani,,unaofuata,lengo nikamuuze kea faida ili nione tu biashara inavyoenda,
Waswagaji Hawa hutembea usiku kucha,
Baada ya kumpa mswagaji napanda usafiri kurudi town,kesho yake naibukia mnada unaofuata,ng'ombe kishafika,namlipa mswagaji buku mbili yake,ng'ombe Nampa dalali auze kwa 350,000,
Hadi mnada unakufa ng'0mbe hajauzwa,kumbe dalali anapandisha Bei auze 370000,apate 20,000 Cha juu,
Ng'ombe kakosa mteja,natafuta mswagaji Tena namkabidhi ng'ombe apeleke mnada mwingine,ila Sasa mchezo nimeanza kuusoma
 
Kesho yake naibukia mnadani mapema,mida ya saa nne,ng'ombe wangu kishafika,,Sasa naona nijaribu kumuuza mwenyewe sihitaji dalali,
Kukukuruka huku na huku mi bado mgeni na ng'ombe sijawasoma naona wote Kama wanafanana tu,Ina maana ukizubaa ng'0mbe akajichanganya naweza poteza,isiwe tabu,namkabidhi dalali auze kwa 280,000,halafu nasimama kwa mbali nikifuatilia,kila nikimuuliza vipi umeuza,anasema jamaa wanadai niuze 230,000,
Wakati nimemnunua 250,000,
Baadae namfuata mteja mmoja aliekuwa akiongea na dalali na kumuuliza,kwani huyo ng'ombe dalali kakuambia Bei gani,anadai dalali kamwambia 300,000,
Namwuulizia una ngapi?,
Anadai Ana 270,000.
Naenda kumnyang'anya ng'ombe dalali baada ya kuchukua 270,000,
Dalali kafume but at least nimeuza kea faida ndogo na nimeshajua mchongo wote
 



Dah inakera balaa...duh mswagaji 2000?cheap...! Sasa hao madalali wamejaa sana kweny zao la karanga..karanga unamuuza 2700yy anauza 3200 zile nyekundu ...kero sana
 


🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣! Hongera uliweza..nxt tym unaweza kataliwa kuuza ng'ombe wako
 
Dah inakera balaa...duh mswagaji 2000?cheap...! Sasa hao madalali wamejaa sana kweny zao la karanga..karanga unamuuza 2700yy anauza 3200 zile nyekundu ...kero sana
Mswagaji anakua anaswaga ng'0mbe wengi,let say 50-60,kwahiyo kwa siku moja anaweza ingiza 100,000.
Zamani niliijua ukinunua unaswaga mwenyewe mguu kwa mguu,kumbe Kuna maspecialist wa kazi hiyo,wewe unanunua na kukabidhi na kudirect tu peleka sehemu fulani na wanajua kila mnada wa wilaya husika Ama kila zizi,,maana wafugaji wa ng'0mbe za kuuza Mara nyingi wanakuwa sehemu mbili tatu maalumu
 

Hapo nimeelewa...!
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣! Hongera uliweza..nxt tym unaweza kataliwa kuuza ng'ombe wako
Kitu nilijifunza,mnadani wengine wanauza bila dalali,uzuri wa biashara ya ng'ombe hutafuti mteja,Bali mteja ndo anatafuta ng'ombe atakamridhisha,so ni suala la kwenda unasimama na ng'ombe wako mnadani,wateja wanakuja kuuliza na mnaanza ku negotiate,
Sasa Kama unaona usumbufu kusimama juani mda mrefu na hauna utaalamu wa kucontrol ng'0mbe au simply hutaki usumbufu ndo unakabidhi dalali akuuzie,wewe umekaa kwa mbali au vibandani unapata moja baridi moja moto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…