BADILI TABIA
JF-Expert Member
- Jun 13, 2011
- 32,767
- 23,198
Hapa sitopata ushauri wa kuufanyia kazi. Nabeba watoto nampekea kule aliko sasa hivi. Ndo nlichowaza mimi. Naimani anaweza akaamua kurudi nkifanya hivyo. Ngoja nijiandae waungwana. Usiku mwema.
Ninyi wote Mliotoa mawazo yenu hapo chini mbona mnaniponda badala ya kunishauri? Embua angalieni tena mlichokiandika. Nimekuja hapa kufarijika kutokana na Majonzi nliyonayo nyie mnazidi kuniumiza.
Asalam Alaykum Waungwana, Naombeni mnisaidie mawazo yenu ili niweze kumrudisha mke wangu aliyeondoka nyumbani yapata mwezi sasa. Tumejaliwa watoto wa wili na ndoa yetu ina miaka 6 sasa. Tulikorofishana nyumbani akaondoka. Mke alikuwa mama wa nyumbani hivo sina hata house girl. Kupika sijui so nawalisha hoteli na junk food wakati wote. Kuwatayarisha waende shule asubui naona kazi nadhani na leo hawatoenda shule. Nahangaika bila mama yao na nimeshajaribu kumfuata kuongea naye imeshindikana. Ramadhani ndo imeshafika hivyo sijui nitafturu wapi. Nimemkumbuka sanaaaaaaa Mke wangu.
Mkuu ndiyo ukae chini na kufikiria ufanyavyo si vizuri. Hivi kwa jinsi ulivyoileta mada ulitegemea watu wakuambiaje?! Nampa pole sana mkeo maana unamfanyika kazi kweli kweli. Badilika!!
My wife is back home now. Nimeongea naye kuhusu kazi za nyumbani nimtafutie housegirl wa kazi kasema nyumba yetu haina kazi nyingi za kufanya hivo hana matatizo. Nikarudia kumuuliza kakataa. Sasa mi nimfanyaje? Lakini yeye ni mama wa nyumbani akishinda nyumbani mlitaka awe anafanya nini? Pia mimi sijamkataza kufanya kazi au kujishughulisha haya maisha ya kushinda nyumbani kayachagua mwenyewe. Karudi tufunge wote ramadhani.
Hapa sitopata ushauri wa kuufanyia kazi. Nabeba watoto nampekea kule aliko sasa hivi. Ndo nlichowaza mimi. Naimani anaweza akaamua kurudi nkifanya hivyo. Ngoja nijiandae waungwana. Usiku mwema.