Elections 2010 Machozi ndani ya daladala


Nyamayao, daladala ilitoka poata 12:30. so labda alitoka kwa ofisi 12 au 11 na nusu mpaka saa 4 bado yupo njiani............. tena kumbuka hiyo ni express maana ni ya buku nauli
 
Tufanye kweli basi kwa kuwachagua wabunge wa CHADEMa na Dr Slaa. Tusifanye makosa tena ya kuwaacha mafisadi madarakani kwa miaka mingine mitani.
 

well said bro/sisy, ni leo tu nimempa lift mama mmoja akiwa na mtoto mgongoni anatokea Mbezi samaki kuelekea Goba
alikuwa na jasho kuanzia kwenye nywele mpaka miguuni,....baada ya kuingia akapata kiyoyozi akapumua pumzi ndeefu sana na kusema hivi bara bara hii ingekuwa ya lami ningekuwa nateseka hivi kweli? tulikuwa watatu kwenye gari,tukammuliza unafikiri ni kwa nini haijajengwa lami? akasema si hawa CCM ndo wanatufanya hivi! wote tukahamaki na kumgeukia na kumuuliza kwa hiyo utampa kura yako Dr Slaa?
alisita baadaye akatujibu kinyume na tulivyotarajia. akasema nitachagua ccm ili waendelee kutufanya masikini tumeshazoea maisha haya!
akaendelea kusema alikuwepo keenja hapa amekula na sasa ameshiba ameacha na kugombea sasa tumeletewa mwingine naye tutampa ale akishiba aende zake.....
mpaka anashuka hakubadilisha usemi wake ila alionekana dhahiri kuwa anachokisema sicho anachokisimamia.....
tulibaki kujiuliza labda ametuogopa akahisi sisi ni watu wa ccm tunamuienjoy.....tulijaribu kumsisitiza amchague Dr Slaa akawa anapinga na kusisitiza kuichagua ccm huku akiiponda kwa nguvu zote.......

....tulichokiona ni kwamba either hawa ndo wapigakura ambao ccm inajivunia au ni uwoga ulitawala vichwani mwa wabongo hadi kuhisi kwamba ukichagua upinzani basi utashughulikiwa.....please wadau kila mtu anapopata opportunity amuelimishe mtu kuhusu upinzani,tusiwaachie walioko front peke yao, i mean wagommbea.
 
Tufanye kweli basi kwa kuwachagua wabunge wa CHADEMa na Dr Slaa. Tusifanye makosa tena ya kuwaacha mafisadi madarakani kwa miaka mingine mitani.

Ni kweli mkuu, yaani tusiache nchi iendelee kuchachuliwa ili hali tupo tunaona!. Tafadhali fahamisha ndugu na jmaa yako aliyepo kijijini.

Majuzi nilifanikwa kufika nyumba ya balozi mmoja katka kijiji fulani, nilihitaji kununua shamba, bac alipo nambia bei kubwa nikapata nafasi ya kumchomeka kwamba wewe mapicha ulojaza hapo mlangoni kwako ya JK na mafisadi wenzie wamemaliza hela zote.. bac tukaunganisha story hapo na mwisho akanambia ukweli kwamba bwan wee.. hii anaweka apate mlo, lakini siku ya kupiga kura anajua mwenyewe atakacho kifanya! aliniacha hoi alipo sema hata hii hospitali ya kijiji wakiumwa wakienda hata panado wanaandikiwa wakanunue! akasema hata chumvi imepanda bei?

Kweli machozi yapo kila kona ya nchi, lakini naamini yatafutia yote baada ya 31 october, kama haki itatendeka!

Na chonde chonde nawasihi NEC tendeni haki, kwani mifanya hivo hata raisi atakaye ingia atawalinda, kwani mtakuwa mmesimamia haki, wala msihofu kwamba kwa kutenda haki kibarua chenu kitaota majani!

 

Hata wewe umeona dada,

Dogo kaandika vizuri sana. Sijui kama kweli watu wanaelewa kinachoendelea. Ila hata kama JK atashinda, kwa jinsi watu wanavyopigika asije kushangaa siku moja wakamfuata Ikulu na kumwomaba atimkie zake Bagamoyo au kwenye mahekalu yake pale Chalinze!
 
Nimekusoma mkuu. Hata mi machozi yamelenga machoni. Lakini nauliza, mbona ile makala yako ya mkutano wa moro na mama wa ndizi ulitumia kiswahili fasaha kuliko makala hii?

ile si yake ilitolewa kwenye gazeti na RAIA MWEMA, na GODFREY DILUNGA
 
Sina la kusema, ila naomba kuuliza je? viongozi wa nchi hii wanasoma jamii forum? manake nadhani hapa ndo mahali muafaka pa kujirekebisha.
 
...............please wadau kila mtu anapopata opportunity amuelimishe mtu kuhusu upinzani,tusiwaachie walioko front peke yao, i mean wagommbea.

Heshima mbele Mkuu...........hayo ndio maneno.........kila mtu amuelimishe mwananchi asiye na uelewa juu ya uchaguzi huu............

ile si yake ilitolewa kwenye gazeti na RAIA MWEMA, na GODFREY DILUNGA
..........kwani umejuaje kuwa Mubezi sio Dilunga..............
 
The trouble with this country is that there are too many politicians who believe, with a conviction based on experience, that you can fool all of the people all of the time.
 
Kuna mchungaji wa Kanisa moja hapa Dsm,jana Jumapili kawaimbisha watu wimbo wa taifa,na pia akawaambia wasali sala ya toba kumuomba Mungu awasamehe kwa kuchagua viongozi wabovu....tupende tusipende,sisi kama wananchi ndio tumefikisha nchi yetu hapa,tuna wajibu wa kuchagua viongozi bora...
 

Dah! unaweza kuangusha machozi kanisani kwa kuimba wimbo wa Taifa kitu ambacho hukukitegemea hata siku moja.
 
Dah! unaweza kuangusha machozi kanisani kwa kuimba wimbo wa Taifa kitu ambacho hukukitegemea hata siku moja.

Kwa mwendo huu naona taifa linaanza kuundwa upya. Yaani bila uhuru wa pili hatuendi kokote!
 
ndio maana narudia kusema hili....LAZIMA SIKU ZA USONI TUWE NA KAUTARATIBU KAKUPIMA AFYA ZA AKILI HASA ZA WAGOMBEA URAIS MIMI NATILIA SHAKA MUONEKANO NA UWEZO WA MGOMBEA HUYO WA CCM, NATILIA SHAKA KAMA KATIMIA, BADO NAFIKIRI KWA MAKINI.
 
Sina la kusema, ila naomba kuuliza je? viongozi wa nchi hii wanasoma jamii forum? manake nadhani hapa ndo mahali muafaka pa kujirekebisha.
Hawasomi lakini kuna mashushushu wao wanaowapelekea taarifa hizi.
 
Na mimi nimekaa muda mrefu kabla ya kuamua kujibu hii thread. Sikuinama lakini nilikuwa naangalia kioo cha computer bila kukiona, sikutoa machozi lakini nilisikitika sana. Nimesikitika zaidi pale ambapo inaonyesha wazi kuwa watanzania tumeendelea na tunaendelea kuwa wadangayika wakati vitu vya ukweli na uwazi juu ya ubovu wa huu uongozi na wanasiasa hawa walioko madarakani wa chama tawala.

Tunazidi kudanganywa kwa maneno matamu na ambayo hayahitaji mtu aliyeenda shule kujua kama kuwa huyu kiongozi wetu hatufai na anatupeleka pabaya. Yes, nasema hayahitaji shule ni sawa na yule Bibi Kizee aliyetoka kijijini huko Pwani kwenda katika gazeti la Mwananchi kusema kuwa Rais amekosea kwa kuwatukana wafanyakazi pale Diamond siku ile ambayo mimi naita ni "Mbayuwayu Day" wakati wazee wengine wako pale lakini walikuwa wakipiga tu makofi. Kwanini tunadangayika kiasi hiki?

Kiongozi anayejigamba kuwa wao ndo walianza kufichua ya EPA, na wao wako mbele kwa kupinga ufisadi, je angeenda kumpigia debe Lowassa na Mramba majimboni kwao pamoja na madudu na kesi walizo nazo (respectively) katika mbele ya uso wa jamii? Lakini bado huko walipigiwa makofi na wananchi. Tuna nini sisi watanzani? Kwanini tunadangayika kiasi hiki?

Tumeshuhudia wote katika mchakati wao wa kuchagua wagombea jinsi fitna na maleno maalumu ya kupunguza kasi ya kambi ya kupambana na uovu bungeni. Je inahitaji kweli kuwa na elimu gani mpaka kujua kuwa Selelii hakuhitajika na chama aingie Bungeni chama kinachoongozwa na Kikwete? Mshindi ameshinda, wanamwengua na wanampa mshindi wa tatu wakimruka wa kwanza hivi tunahitaji macho mangapi kuona hapo? Kwanini tunadangayika kiasi hiki?

Tumeona Mwakalebela alivofanyiwa Iringa, na kabla Kikwete hajaenda kule alionekana yumo kwenye msimamo lakini alipofika akapandishwa jukwaani kumpigia debe mpinzani wake, hii inaingia akilini watanzania? Mtu uliyemuengua kwa rushwa unampandisha jukwaani kusupport chama haisomi kwenye kichwa changu kabisa. Kwanini tunadangayika kiasi hiki?

Nasema hivi kwa kuwa kwenye hadithi hii, inaonekana huyu mama na huyo mzee aliyepitilizwa kituo akaja kushuka baadaye wote walikuwa na mpango wa kumpigia kura Kikwete kabla ya kupanda katika hilo gari. Je walikuwa bado hawajajitambua kuwa wanadanganywa? Mama mpaka wamegusa hali aliyonayo ndo anakumbuka kuwa huyu mtu siyo? Je tusubiri mpaka ufeel kuwa unakuwa affected personally na physically ndo ushtuke? Kwanini tunadangayika kiasi hiki?

Athari zingine sio lazima zikukute wewe personally au wakati mwingine unakuta zinakukuta ila indirect ila kwa sababu tu huwezi kuchambu kwa nini yamekukuta huwezi kutambua yamesababishwa na utawala mbovu.

TUBADILIKE NA WAKATI WA UKOMBOZI NI SASA!!
 
Nyie lieni tu wao wanajilia vyao

Dk. Chegeni amwaga ambulance jimboni


na Sitta Tumma, Magu


MBUNGE wa Jimbo la Busega, Dk. Raphael Masunga Chegeni (CCM), amekabidhi magari mawili ya kubeba wagonjwa (ambulance), yenye thamani ya zaidi ya sh milioni 110, katika vituo vya afya vilivyopo jimboni humo.

Magari hayo yamekabidhiwa mwishoni mwa wiki katika vituo viwili vya Lukungu na Nyashimo Nassa na kufikisha idadi ya magari manne ya wagonjwa jimboni humo.

Akikabidhi msaada huo, kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Cornel Ngudungi na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Bonaventura Kiswaga, Dk. Chegeni alisema lengo la msaada huo ni kuwasaidia wananchi wa jimbo la Busega kuwa na huduma ya usafiri wa uhakika.

"Vituo vya afya vinavyokuwa na magari ya kubeba wagonjwa inasaidia sana, na mimi leo nakabidhi magari haya mawili kwenu! Kwa maana hiyo nimekamilisha ahadi nilizowaahidi wananchi wangu", alisema Dk. Chegeni.

Magari hayo ya wagonjwa yana vifaa vya kisasa vya kliniki, pamoja na kifaa kikubwa cha kupima ugonjwa wa moyo, na kwamba msaada huo umetolewa na marafiki wa mbunge huyo wanaoishi nchini Uingereza.

Kwa upande mwingine, Dk. Chegeni aliwaasa wananchi wa jimbo hilo kuwa makini na watu wanaopitapita kuwalaghai wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…