Serikali ni ya kulaumiwa 100% lakini na sisi WABONGO tubadilike jamani, tujifunze utamaduni wa wenzetu, tusiisubiri serikali, kila mmoja atimize wajibu wake. Let's all get involved in making a change for God sake! Sisi tumezidi kulalamika bali hakuna vitendo!Tofauti yetu na mzungu ama mtu aliekulia utamaduni wa Magharibi ni kwamba mzungu mara baada ya kuona kitu kama hii, anaingia kazini yeye binafsi kutafuta ufumbuzi na kutoa msukumo unaotakiwa, iwe ni celebrity, mwanafunzi ama hata mtalii wa kawaida lakini sisi wengi wetu tunakimbilia kupayuka tu. Zhule na wengineo suluhisho wakati mwengine sio kusubiri Serikali, ukiona hali kama hii jiulize na wewe sio serikali tu, nini unaweza kufanya kusaidia?
Nakupa mfano mdogo endapo hali kama hii angeliiona gap year student kutoka UK, angeweza kueneza habari kwa madhumuni ya kuchangisha hela na likajengwa japo darasa moja pengine baada ya mwaka, Sasa kama wenzetu wao wana mwamko kama huu kwa nini sisi tushindwe?
Kama kwa mfano mwengine wiki iliyopita kulikuwa na charity appeal ya kuchangia disadvantage children wa UK (BBC children in need) na wanaochangia wengi ni wananchi wa kawaida kama wewe na mimi, hela inayopatikana inasaidia miradi mbalimbali ya hawa watoto, iwe ni huduma za afya, elimu nk. mwaka huu pekee walichanga kiasi cha £20,309,747 ikiwa wastani wa pauni millioni 20 kupatikana katika siku 2 tu!!!! Sio kama nataka kufananisha wao na sie ila kwa nini na sisi tusiwe na walau vijiharambee vidogo kama hivi? Si tunaona watu wanachangia vitu vya kibwege kama BSS na big brother? mfano mdogo iwapo kutakuwa na appeal kama hii na kila mtu atapiga simu ama kutuma text kwa gharama ya shs.500, watu 20,000 pekee zitapatikana shilingi millioni 10,000! Tosha kujenga madarasa walau matatu.