Filipo Lubua
JF-Expert Member
- Nov 18, 2011
- 339
- 578
Ni machungwa ya Muheza, yenye sifa kemkem
Yamejaa kila muji, hakuna asoyajua
Yanauzwa bei chee, na fukara anamudu
Ni machungwa tamanika, bali ndani yameoza
Yanazidi ya handeni, yamenea nchi nzima
Sio Dar na Arusha, hata Mwanza yashafika
Yauzwa barabarani, wa malori ni wateja
Ni machungwa tamanika, bali ndani yameoza
Hayauzwi mchanani, usiku ndo mudawe
Wachagua upendalo, moja lakutosheleza
Huwezi kulala njaa, hayuzwi kwa pesa nyingi
Ni machungwa tamanika, bali ndani yameoza
Walaji wafakamia, tena wala na maganda
Hawajali zao afya, hawajali kuendesha
Tena walia gizani, hata maji hawaoshi
Ni matamu ya Muheza, bali ndani yameoza
Ukifika Dasalaam, yamejaa Buguruni
Ukenda uwanja wa fisi, hapo ndipo soko kuu
Kuna bei za jumla, rejareja utapata
Ni matamu ya Muheza, bali ndani yameoza
Arusha yapo Mrina, hata Naaz yamejaa
Ukifika usiseme, yenyewe yatajileta
Chukua la chapuchapu, au kalye hotelini
Ni matamu ya Muheza, ila ndani yameoza
Huko mwanza yamejaa, kila kona utaona
Wateja waongezeka, vijana hata wazee
Haya machungwa jamani, kwani yana ladha gani?
Ni matamu ya Muheza, ila ndani yameoza
Watu wamedanganyika, kununua ya Muheza
Ya nyumbani hawapendi, wanasema ni machachu
Mwishowe wanajutia, miharisho ianzapo
Ni matamu ya Muheza, ila ndani yameoza
Wateja hawambiliki, wanakula na uozo
Wanadai yanakidhi, kwenye njaa ya haraka
Chalinze ukiyaona, hata wewe tatamani
Ni matamu ya Muheza, ila ndani yameoza
Abudula wa Tabata, nalia nimkumbukapo
Alisema ni matamu, halali bila kuyala
Mwisho yakamsulubu, yakamfanya kijiti
Ni matamu ya Muheza, ila ndani yameoza
Nilimwonya mara nyingi, asiyale si salama
Ila ye akakaidi, akaona namghasi
Akatoa fedha zake, akanunua kwa pupa
Ni matamu ya Muheza, ila ndani yameoza
Abudula akayala, mwisho kaanza endesha
Kamfunza na mkewe, naye akawa dereva
Wote wakaanza endesha, chanzo hayo ya Muheza
Ni matamu ya Muheza, ila ndani yameoza
Walimwengu sikieni, si salama aya machungwa
Ningekuwa mwenye nchi, marufuku ningepiga
Yasingeuzwa nchini, na masoko ningefunga
Ni matamu ya Muheza, ila ndani yameoza
Tatizo ni moja kubwa, na watawala walaji
Watokapo ofisini, gulioni wapitia
Wanunua mojamoja, tena ya bei ghali
Ni matamu ya Muheza, ila ndani yameoza
Sikiza usikiaye, sishupaze shingo yako
Machungwa ya kununua, sio haya ya Muheza
Mbona mazuri yapo, kwani situnde mwenyewe?
Achana na ya Muheza, katunde nyumbani kwako
© Filipo Lubua, Nov. 30, 2012