Macron kutoa heshima kwa wanajeshi waliouwawa Niger

Macron kutoa heshima kwa wanajeshi waliouwawa Niger

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa anatarajiwa kusafiri kwenda Niger kwa ajili ya kumbukumbu ya heshma kwa wanajeshi 71 ambao waliuwawa kwa shambilizi la wenye itikadi kali, mapema mwezi huu. Macron atajumuika katika hafla iliyopangwa kufanyika mwishoni mwa juma mjini Niamey ambapo atatoa heshima yake kwa wanajeshi hao waliowawa wakiwa katika kambi ya kijeshi katika eneo la Sahel.

Tukio husika lilitokea katika Desemba 10 katika mkoa wa Tillaberi. Aidha pamoja na tukio hilo Macron atakutana na Rais wa Niger Mahamadou Issoufou mjini Niamey. Viongozi hao wawili wanatarajiwa kuzungumzia mkutano wa kilele wa Januari 13 wa mjini Pau nchini Ufaransa, ambao utayakutanisha mataifa ya Burkina Faso, Mali, Chad na Mauritania.

Ufaransa ina jumla ya wanajeshi 4,500 katika maeneo ya mataifa hayo ambapo kwa takribani miaka 7, wamekuwa wakikabiliana na makundi ya wenye itikadi kali.
 
Back
Top Bottom