Mada maalum kwa wachoraji, sanaa ya picha na rangi

Kwa hiyo haya yooote umeongea ili kupinga kuwa hakuna picha za kuedit siyo,
Haya tufanye hakuna picha za kbumba kwa apps nk,halafu tuone itawasaidia nini watoto zetu wanaotamani kuinua vipaji vyao,
Tufanye mm sina kipaji cha uchoraji ndo maana nasema si kila picha inayoletwa humu ni halisi,
 
MI SIO MCHORAJI ILA KAMA UNABISHA NTAKULETEA VIDEO ZA MTU AKICHORA HADI KUMALIZA MCHORO
Nini unachodhani nabisha,
Narudia kusema siyo kila picha unayoiona ni ya mkono mtupu,picha nyingi sana huwa zinaeditiwa,
Kinachofanya ukatae ni ile tabia ya kitanzania ya kutaka kuonesha ujuaji siyo usahihi,maana unaongea utadhani nilichosema ni PICHA ZOTE HIZI NI EDIT,
Kuniuliza km sijawahi ona MTU anachora hatua kwa hatua ni kunitukana maana wewe uliina ila mimi huwa nafanya,
 
HAYA...
 
Kuna jamaa yangu ni bingwa wa kuchora picha za vinyago(tingatinga)nk lkn ukimpa picha hata ya paka anashindwa,lkn na yy huwa anapeleka sana nje kazi yake ya kuchora picha za vinyago,kumbe kwenda kuonesha kazi nje siyo kujua usahihi wa kuchora picha halisi,
 
Mimi nitoe ombi moja,tena kwa moyo mkunjufu,
Tutumie kurasa hii km sehemu ya kupanuana kuinuana na kuoneshana njia siyo sehemu ya kubishana na kujivuna na kuonesheana umaarufu,
Humu kuna vijana wadogo wanahitaji kufika juu zaidi hata ya tulipo,yafaa tuwaoneshe UHALISIA na njia halisi ya sanaa hii kupitia mazingira na vifaa halisi vinavyopatikana mitaani kwetu,
Kumuonesha mtoto anaejifunza kitu ambacho hata mtaani hakipati ni kumkatisha tamaa na kumvunja moyo,
Tuwaambie kuna picha edited,kuna apps za kuchora na kutengeneza picha,kuna picha halisi za mkono mtupu na rangi ama sketch ya penseli tu,tena penseli hizi hizi za kichina,
Tukiwaambia kuna penseli maalumu ama rangi maalumu ama chochote maalumu ambacho mtaani hakipo tunaua vipaji vyao,km mtaani kiuhalisia tunachora kwa matope,tunachora kwa manyoya ya punda tuwaambie na kuwaonesha,wakivuka hapo watajiongeza kutafuta vifaa ama mbinu za zaidi ya hapo,
A to B siyo A kisha Z
Tuwaoneshe kazi halisi zetu za mikono
Tuwaoneshe njia na changamoto,
Tutakuwa tumetenda haki,na tutakuwa tumerudisha shukrani kwa Mungu aliyetutunuku vipawa hivi,
 
Da mkuu umenichekesha sana eti hata paka hawezi kuchora
 
Da mkuu umenichekesha sana eti hata paka hawezi kuchora
Kuna kuchora picha za taswila halisi,na kuna kuchora picha za vinyago yaani image isiyo halisi(tingatinga,katuni nk),
Halafu kuna kuchora maumbo ya kufikilika ya vitu ambayo hunakshiwa kwa rangi,na kuna kuchora mandhali,
Wapo watu wanachora maumbo tu na kuyapaka rangi nao wanauza nje na wanajiita wachoraji,
Wapo wengine wana nunua picha za wasanii chini na kuzipeleka nje lkn hata kikombe hawezi chora na anaweza jidai anajua sanaa,
Lkn yote haya hayana faida km hatutaonesha kazi tunazofanya na kufundisha/kufundishwa hatua ili wengine wajifunze ama kuhamasika,
Nawasifu sana wachoraji wa kitanzania wa mtaani maana wanachora kwa kutumia kalamu za kawaida kabisa,canvas na undercoat za kawaida kabisa,kwa hali ya kawaida na zinakuwa bomba sana,sana,
Ndo maana kuna wazungu wanatoka huko huko waliko hao mnaodhani wachoraji wakubwa na wanakuja kununua ama kuchorewa picha mbagala
 
Nimekuelewa mkuu
 
Unaposema picha za ku edit unazungumza kuhusu nini?

Binafsi nachora fine art....
Nafanya Abstract......
TINGATINGA...
Landscape... .
Wildlife animal n. K

Natumia Acrylic, Rangi za mafuta, rangi za maji, na painting technique nyingine... Nachora kutumia Canvas, Manila paper, Hardboard n.k....

Pia nachora kwa Penseli, Kalamu ya Wino I mean Sketching iwe rough sketching kwa ajiri ya finishing ya Rangi mpaka full complete sketching bila rangi.... Pia Nna chora kwa kutumia Computer au Simu kwa kutumia special software ama app.....

Sijawahi kusikia kitu kinachoitwa picha za ku edit...... .
Labda ni Tecnologia Mpya, emu nisaidie kujua, picha za ku edit ndo picha za aina gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…