Mada maalum kwa wanandoa



Hahahahaaaa! Kuoa bila mipango au kulenga ishu moja tuu matokeo yake ndiyo hayo!!

Kabla ya kuoa ulipaswa kujua au kujifunza utaishi vipi na mkeo na hata baadae wanao! Yanayobaki muachie Mungu

Mie nina zaidi ya miaka 10 kwenye ndoa, mwanzoni nilipata ugumu flani coz kuna mmoja wetu kabadili dini so kufundishana na kuwekana sawa ilikuwa shida kidogo! Pia nilikiwa mnywaji, kurudi usiku hakuna muda na familia napo vilichangia kuweka gap kwenye ndoa yangu na wakati huo kipato kilikuwa chini, so tukawa na matamanio yasiyotimia matokeo yake ni stress na kugombana!

Kabla ya kuoa nilipanga kuwa na familia yenye furaha, outings na vacations na safari ni vitu napenda sana kiukweli!! Nilihitaji mtu wa kufanana nae!

Nilipoanza kazi na NGO moja hivii inadeal na maswala ya ndoa! Nilikuja kugundua visababishi vya vikubwa vya migogoro ya ndoa ni nini! Kimoja wapo ni kitendo cha kila siku kurudi nyumbani usiku wa manane, umelewa wanawake wanaumia sana ila basi tu! Yakimzidi ndipo nae hutafuta faraja kwa namna ingine au hubadilika tabia na ndipo hapo, migogoro inaanzia!

Niliamua kubadilika, pombe nikaacha na familia yangu ikawa ndiye rafiki zangu wakubwa!!

Naishi kwa amani na nafurahia maisha ya ndoa to maximum!! Sijutii kwa hakika na naamini hata mke wangu vile vile!!

Tunatoka outing wote, tunasafiri tunavyopenda tunafanya yanayotupasa yaan ni full furaha! Namshukuru Mungu kwa kweli.

Ndoa ya furaha inawezekana ila kwa jitihada za pande zote mbili!! Ukiona unaleta furaha ila upende mwingine hauhitaji uwe hivyo hilo ni tatizo na hapo inabidi kuchukia hatua!

Kikubwa tumia muda mwingi kuchunguza utayetaka kuoa au kuolewa nae. Kama ana tabia usiyoipenda jikatae mapemaaaa! Usitarajie atabadilika akishaingia kwenye ndoa, na hili ndiyo kosa la wengi!!
 


Unataka kuniambia kuwa hajioni kama anajiharibu mpaka mimi nimwambie? Ndani kuna vioo kila sehemu, chumbani, vyooni, bado tu mpaka mimi nimwelekeze what to do? Wanawake walivyo wa hajabu, mimi kama mumewe ninaweza kumuambia what to do ili asijiharibu shepu, yeye ataanza kufikiri labda nina nyumba ndogo au kuna mwanamke mtaani namtamani alingane naye, ndiyo maana unakuta sie wanaume hatuwaambii chochote wake zetu kuepuka malumbano ya kijinga. Unamwacha ajiharibu zaidi ili upate kisingizio ama kigezo cha kutafuta nyumba ndogo. Endeleeni kujiharibu tu na kutukata stimu ya kutowapenda.
 
Mbarikiwe sana wanaume wote ambao familia zenu ndo priority zenu

Mwanaume anaspend muda mwingi bar na marafiki kuliko anavyospend na familia yake. Kila siku unarudi usiku wa manane, familia yako unamuachia nani? Huwa inanichosha kwa kweli kuwa wavulana wasiotaka kukua, mtu ameoa ila anataka aendele kuning'iniza miguu bar kama paka na kurudi usiku as if hana watu wanaomuhitaji nyumbani. Siku akipata shida, wakesha bar wenzie huwaoni, ni familia inayosuffer. Sijui kwa nini watu hawajifunzi kuwa hata ukifa wasifu wa marehemu hautosema "marehemu ameacha marafiki 5 aliokuwa anakesha nao bar".

It hurts watoto wanamuona baba labda asubuhi tu wakiwa wanakwenda shule. Bado mama hawezi kulala kwa amani hadi mume arejee nyumbani. Unamtesa mkeo kukesha kukusubiri, afu ndo mtu anaingia mdomo unanuka na anataka kukugusa ptuuuu. Me ujinga wa kuamka saa 9 kumfungulia mlango mtu aliyekuwa kwenye starehe zake nilishasemaga sitosettle for that. Wavulana mbadilike
 
Katika vitu ambavyo siwezi kuishi kwa kukosa Amani nmekubari matokeo siku nyingi ndoa imenishinda nmemuachia nyumba na mtt moja mwingine naishi nae mwenyewe bahati yngu nafanya kazi njee ya nchi nikija likizo kwa miaka 2 mara moja nafikia hotel mwenzi wngu moja nasepa kosea vyote ila ukikosea kuoa au kuolewa ni balaa kuliko kitu chchote duniani usije kbs kutoa lawama ukisikia mtu amejitoa Uhai ndoa zina mengi jamani...

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Jifikirie we ukitaka kuvaa nguo kama hajakuchagulia yeye hajisikii vizuri tena wakati mwingine anakukataza usivae nguo fulani wakati wewe ushaitoa kabatini uivae, ndo vivyo hivyo na wewe unatakakiwa umwambie kama mwili alionao kwasasa haukuvutii tell her and advice accordingly. usiache hadi wenzie wamwambie. Acha uoga wa kusema sijui mtalumbana we muulize wakati nakutongoza lile umbo lililonivutia ndo nataka uwe nalo.
 
Oooh lala Love in the air...........😉😉

Hello Mnama, habari ya siku nyingi...??

Kwema??

Kasie na Mahaba yake as usual hehehehee, niko vilevile bado hata sijaacha.
 

Umeandika ukweli mtupu, kila anayeoa anatarajia amani na furaha humo ndoani, ila anayokutana nayo ndiyo humfanya ajutie kutia maguu humo


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hello Mnama, habari ya siku nyingi...??

Kwema??

Kasie na Mahaba yake as usual hehehehee, niko vilevile bado hata sijaacha.

Poa kabisa pande hizi za kanda ya ziwa pembezoni mwa lake Victoria............

I can see for sure the one and only....... hope one day....
 
Huhuuhuuhh[emoji13][emoji13][emoji13]...eti lazima nyongo ijae mwilini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…