Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Hivi Mshana naweza kupata software za ku diagnosis magari hasa aina ya Toyota ili kujua tatizo la gari ili nikienda garage nimwelezi fundi nini cha kufanya sio aanze kukisisia tu na kama zipo zinauzwaje?
 
Msaada wa mawazo kwenye Hyundai Tucson CC1998 ya mwaka 2006, hasa kwenye upatikanaji wa vipuri, ughari wa matengenezo yake(service cost), ulaji wa mafuta na urahisi wa upatikanaji matengenezo. Mawazo yenu mhimu kabla sijadumbukia shimoni. Shukrani
 
Nataka kununua gari aina ya Suzuki escudo/Nomade,tafadhali nishaulini model gani inanifaa na je gari hii itanifaa kwa familia na pia inagharimu kiasi gani from japan to home?
 
Habari zenu, msaada tafadhali........
Naomba kufahamishwa juu ya tofauti ya ubora wa toyota hiace yenye engine ya 3l na toyota hiace yenye engine ya 1kz.
 
Zipo garage zenye hiyo mitambo
 
batamaji kuna garage zenye hizo software na ni vitu vya kitaalam kwakuwa kinachosoma ni codes kwamba code fulani ikitokea ni tatizo fulani , kuna kautaalam kanahitajika. Hebu jaribu kuwasiliana na RRONDO
 
Last edited by a moderator:
Msaada wa mawazo kwenye Hyundai Tucson CC1998 ya mwaka 2006, hasa kwenye upatikanaji wa vipuri, ughari wa matengenezo yake(service cost), ulaji wa mafuta na urahisi wa upatikanaji matengenezo. Mawazo yenu mhimu kabla sijadumbukia shimoni. Shukrani

Ni gari ngeni Tanzania ila za kisasa hivyo ni wachache wenye utaalam nazo
 
Nataka kununua gari aina ya Suzuki escudo/Nomade,tafadhali nishaulini model gani inanifaa na je gari hii itanifaa kwa familia na pia inagharimu kiasi gani from japan to home?
 
et wakuu gari yakutumia diesel si inaweza shtuliwa ikawaka bila battery?

Hahaha Umeikumbusha kitambo sana mkuu, hilo jambo tumewahi kulifanya ila kwa sasa magari yana umeme mwingi sana sidhani kama inawezekana
 
1KZ ni engine bomba sana

Vipi kwa ajili ya biashara ya daladala maana mie nipo Mwanza na huku mafundi wanadai 3l na 5l ndo zinastahimili. Vilevile ndo zipo nyingi ktk biashara hii. Pia nikiangalia bei naona 1kz zina bei nafuu kuliko 3l na 5l lkn hazitumiwi sana kwenye biashara.
 
Hizo zinapendwa kwasababu ulaji wake wa mafuta ni mdogo kulingana na 1kz
 
Mkuu mshanajr et al..naomba kujua mazuri na changamoto ya kagari kanaitwa duet
Shukrani.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mshanajr et al..naomba kujua mazuri na changamoto ya kagari kanaitwa duet
Shukrani.

Changamoto yake kubwa ni vile kanaitwa ka babywalker lakini mengine yote kako vizuri mno kuanzia ulaji wa mafuta ubora wa engine na gearbox, uimara wa body, speed na upatikanaji wa vipuri.... Kachukue kama bado hutajutia
 
Last edited by a moderator:
Changamoto yake kubwa ni vile kanaitwa ka babywalker lakini mengine yote kako vizuri mno kuanzia ulaji wa mafuta ubora wa engine na gearbox, uimara wa body, speed na upatikanaji wa vipuri.... Kachukue kama bado hutajutia

Havome a.k.a thanks- bro mshana
 
Last edited by a moderator:
wakuu habari naomba kujua uhimara na ubira wa haya magari
TOYOTA RUSH Vs TOYOTA RAV4 OLD MODERI
 
nashukuru kwa kuleta huu uzi mhimu sana hapa jukwaani. Naomba kujua changamoto za kiufundi au mapungufu au matatizo ya gari aina ya Townace Noah kama unayafahamu. Nategemea kulinunua ambalo limetumika hapa tz na limetembea Km 35,000 tu. Nitegemee kukutana na changamoto gani? natanguliza shukrani
 
Hazina makuu zaidi ya changamoto za kumiliki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…