Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Jaribu kubadilisha ECU huwa haisomi upande wa gear yan muite fundi ajaribu kufunga ECU nyingine uone kama itafanya kazi, hapo ECU itakuwa haina mawasiliano mazuri na gear box
 
Habar za mapumziko ya Karume Day? Naomba ushauri wakuu, navua matairi kwa mara ya kwanza!
Naomba kujua nivae size ipi na aína gani kwa uimara na ubora hapa kwetu Bongo nchi ya majaribio kila leo!
Size nilizokuwa nazo toka Japan ni 185/70R14 88S!
Asanteni sana kwa huduma hii nzuri!
 
Weka hiyo hiyo usibadili
 
Ni gari aina gani? Jaribu kufuatilia vzr specs za gari yako. Mm niliwahi nunua gari yenye specs tofauti na tairi za gari hivyo nikabadilisha tairi ili kuweka zile zenyewe.

Ukiweka aina ya gari itakusaidia kukupa jibu sahihi usiamini sana size ya tairi zilizokuja na gari
 
View attachment 335556

Hiyo ni tairi size 17 ambayo ilikuja na gari lakini sio size proper. Gari hii ni escudo 2007 ambayo appropriate size ya tairi ni size 16. So imebidi kuvua rim na kuweka rim za 16 tofauti na zile 17 zilizokuja na gari
Hii ni michezo ya kwenye meli mjep hawezi kufanya hivyo
 
Gear box oil ya gari gani kwanza ? Kama ni za automatic gearbox za gari za kijapan, huwa haitumii oil bali ATF ( Automatic Transmission Fluid ) waswahili tunaita hydraulic oil, inabadilishwa kila baada ya Km 100,000 ( Laki moja ).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…