Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Msaada jamani Raum inaonesha hivi kwenye Dashboard
Hiyo ni kama master warning sign.

Kuzima kwa hiyo sign ni hadi warning signs zote zizime kwenye display iliyo mbele ya steering. Hata usipofunga mkanda lazima iwake.

Kwenye hiyo display iliyo mbele ya steering kuna taa gani inawaka?
 
Mkuu hiyo ni boot rubber ishakufa ni ya kubadili pitia na kiyo CV joint kama ni nzima,he gari yako haina mlio wa ka! Ka! Ka ukatapo kona nyingi
Ndio inalia hivyo nikikata kona, sasa limepaki tu. Napataje spare na wapi wanauza na bei zikoje ni Honda CR-V
 
Ndio inalia hivyo nikikata kona, sasa limepaki tu. Napataje spare na wapi wanauza na bei zikoje ni Honda CR-V
CR-V zilikua zinazisumbua spares enzi hizo, ila nina imani siku hizi zinapatikana. Kuna mdau aliwahi weka namba yake huku, hebu jaribu kucheki nae 0712 183826
 
Kwenye gari yangu Verosa hakuna hiyo od(overdrive) button sasa hii maana yake nn?
 
Wajuzi...nijuzeni...kati ya nissan sunny na honda jazz ipi gari murua kwa matumizi ya mjini mjini?!
 
Mwenye uzoefu na mark 2 gr anipe uzoefu kuhusu uimara, fuel na spare zake kwa ujumla...natanguliza shukrani.
 
Mwenye uzoefu na mark 2 gr anipe uzoefu kuhusu uimara, fuel na spare zake kwa ujumla...natanguliza shukrani.
Inategemea kuna six na four cylinders... Hapo swala la fuel limepata ufumbuzi uchague ipi.
Kwa bodi Grand ni mkorosho unatengenezeka na spare zake nafuu.
NB:uimara wa gari sometimes ni matumizi yako mwenyewe. Unazingatia services... Unaliendeshaje kama rally au unaenda harusini vyote hivi hufanya gari iwe imara au la.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…