Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

"Wadau nina Passo piston 3 nataka kubadili engine kuweka ya piston 4. Naomba kujua gharama ya tukio zima kuanazia manunuzi kwa wanaoju. Thanks"
Jamaa aliuliza hvyo hapo juu
Simshauri kabisa hivi vitu vinaenda kwa mahesabu yake
 
huu uzi una manufaa sana.nataka kununua honda fit.naomben ushaur juu ya ubora na changamoto zake.asanteni
 
Kwa kujazia ulipoishia mdau, na kumsaidia alieleta shida hio, Toyota Cresta Super Lucent, Mark II Chaser, Matk II Blit na zote zinazotumia injini ya 1G ama VVT-i, inapotokea gari ikakatika timing belt usiilazimishe kuiwasha. Unapoendelea kupiga starter ikiwa haina timing belt (mzigo) inaua valve. Kwa hiyo utashangaa shida ndogo kama ya timing belt inakupelekea kufungua cylinder head yote ili kuondoa valve zilizopinda baada ya kulazimisha kuiwasha. Si wengi wana elimu hii. Hata kwa magari mengine, si busara kuendelea ku start ikiwa timing belt imekatika. Nawasilisha!
 
Nataka kujia kama Discovery 4 diesel zinashida gani maana nimeishakuwa na mapenzi nayo
 
Nataka kufahamu kuhusu volts uimara wake, ulaji wa mafuta na spare. Vipi niandae budget ya shilingi ngapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…