Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Oky kaka mshana jr. Nikijikusanya ntakustua unitafutie mwana jf mwenzio

Karibu sana wengine magari mapya na bomba kabisa wanayapatia kwenye minada bandarini kwa bei poa kabisa ukiwa tayari niambie tuu
 
Kaka Mshana kwa hyo 4m or 5m unaweza kupata gari jipya kwenye hyo minada ya bandarini?
 
Kaka Mshana kwa 4m or 5m unaweza pata gari jipya kwahyo minada ya bandarin?
 
Brevs jamaa anaiuza kutoka tanga to dsm anakula wese mara 3 ni hatari kwamaisha ya mtanzania

Huyo dereva huenda hajui matumizi ya gear! (OD)

Katika hali ya kawaida huwezi kujaza full tank mara 3 kwa km 350!
 
Msaada wadau gari yangu taa ya mafuta inawaka muda wote haizimi licha ya kwamba mafuta ni yakutosha,tatizo limeanza leo jioni baada ya kutembea mchana wote nikapaki, kuja kuiwasha naona taa ya mafuta inawaka nikajua itazima wapi hadi nafika home bado inawaka... Gari Rav 4 Old Model ,Msaada Plz
 

Boya la fuel pump limejam
 
jambo wadau.
Nina toyota hilux inatumia engen ya 3y. Ilianza kutoa mlio na kugonga kwenye mashine mafundi wakaifungua hivyo nikafanya overwhol na ikachongwa size 25.
Mashine imeshafungwa na kila kitu kiko ok tatzo imepoteza nguvu kabisa na inachelewa kuchanganya. Ukiwasha na kupga resi iko poa ishu haitembei unakanyaga mafuta inaenda kwa kusinzia. Bado iko kwa fundi hebu nipeni idea vitu vya kuangalia. Plugs zote zinachoma vizuri
 
jambo wadau.
Nina toyota hilux inatumia engen ya 3y. Ilianza kutoa mlio na kugonga kwenye mashine mafundi wakaifungua hivyo nikafanya overwhol na ikachongwa size 25.
Mashine imeshafungwa na kila kitu kiko ok tatzo imepoteza nguvu kabisa na inachelewa kuchanganya. Ukiwasha na kupga resi iko poa ishu haitembei unakanyaga mafuta inaenda kwa kusinzia. Bado iko kwa fundi hebu nipeni idea vitu vya kuangalia. Plugs zote zinachoma vizuri, taa ya oil inazima yan ishu ni power. Transmision ni automatic na oil yake iko ok
 
Hello guys nauza gari Chaser mayai 2.85M ni mzima inatembea engine standard, cren shaft standard na block pia standards ila inadaiwa MV, gari ipo Dodoma, ukiitaka ni PM, kwa pics, mie mgeni humu so Sijajua ku-upload pictures
 
solution nilisubilie litakaa sawa au nipeleke kwa fundi?Msaada Mshana Jr plz

Ni vema ukaipeleka kwa funding haraka kwakuwa itaunguza sensor ya hiyo taa na hata pump yenyewe
 


Mmh mbona kama umeshairoga hiyo engine? Cheki na funding mzoefu aone nguvu inapotelea wapi, kwa vyovyote kuna shida mahali
 
Kwa wapenzi wa mziki mzuri na mzito lakin gari yako haina buti yakutosha ili uweze kuweka box kubwa la spika nazani hii dizain ya spika zitawafaa sana
 

Attachments

  • 1430548722968.jpg
    16.4 KB · Views: 303
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…