Mada maalum ya mazoezi na kupunguza uzito (fitness and weight loss)

Architect E.M

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Posts
1,222
Reaction score
1,425
Habari wadau. Natumaini hamjambo.

Nimanzisha uzi huu maalum kwa wapenda mazoezi woote na wenye nia ya kupunguza uzito. Tunaweza kushirikishana mambo mbali mbali ikiwemo aina nzuri ya vyakula, aina nzuri ya mazoezi kulingana na umbo la mtu na jinsia yake.
Watu kutoa ushuhuda wa weight loss journey walizopitia, changamoto na namna walivyofanikiwa.

Mimi nianze kwa kutoa ushauri mmoja tu wa kwanza. "CONSISTENCY". watu wengi nikiwemo mimi mwenyewe hua tuna ari kubwa sana ya kuanza mazoezi, lakini tukifika katikati tunakata tamaa au kuishiwa na shauku / ari (burning desire). Ni vyema ukiweka nia, ukaitimiza kila siku. Hata kama ni kutembea kwa dakika 10 kwa siku, ila jitahidi uifanye kila siku. Na ninauhakika malengo makubwa zaidi yatafikiwa.

Karibuni wadau kwa michango mbali mbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…