MADA: Tatizo la Watoto kuchelewa kuongea. Ni kipi chanzo chake? Je, nawezaje kutatua tatizo hili?

Asante sana kwa maelezo mazuri mkuu Ramark ila naomba nikuulize,huko kukatwa ulikatwa ukiwa na umri gani kaka!
 
Mpeleke haraka akakatwe udata na mimi yalinikuta hayo nikaenda Muhimbili wakasema hakuna tatizo nilimpeleka huko akakatwa na sasa anaongea vizuri
Mkuu ulimkata akiwa na umri gani?
 
Mchanganye na watoto wa kiswahili tu mtaani ataweza.. we unamfungia kilasiku ndani hachangamani na watoto wenginewategemea ataongeaje!!
Mmhhhh.... Jina lako hatari sana Mkuu
 
Pole sn mkuu,kwa tatizo hilo la mtoto wko.turudi katika hoja.
Kuto onge mtoto kuna sababishwa na mambo mengi mkuu.

(1)mbele ya ulimi inawezeka kuna vidoti vyeusi ambavyo vinasababisha ulimi kua mzito,na hushindwa kutamka maneno kwa ufathaha.

(2)chini ya ulimi kunakua na uzi ulio shikamana na ulimi karibia ufike mwisho.ukiwepo uzi huo mtoto anaongea kwa shida sana.

(3)NI maumbile tka kwa mola wetu, mjuzi.
UDATA..ni huo uzi uliopo chini ya ulimi,na tiba yake ni kuukata,nenda k/koo mtaaw Udoe,ulizia kabati.au muone doctar KOYA mtaa wa manyema
 
Pole sana hilo ni janga la weng mi pia wangu ana miaka 3 na miez 5 sasa kuongea kwake ndo hvyo hvyo maneno machache kama mtt wa mwaka nilimpeleka na mimi hospital zote wanasema hana tatizo nikampeleka shule ameanza kuimprove kidogo ila bado na kwa speech therapist hudhuria...sema mkazanie tu na shule acheze na wenzie ataongea muda ukifikia ni ulimi mzito tu wtt wanatofautiana
 
Asante sana kwa ushauri ndugu...
 
Nashkuru sana mkuu...inaumiza sana nafsi unapomuona mwanao anajaribu kukueleza kitu akiwa na furaha kisha wewe huelewi naye anategemea umjibu basi unabaki kujichekesha nayeye anabaki kukutizama usoni...ah ila ndiyo maisha tutafanyaje!
 

Shukrani mkuu,huyu jamaa Kabati nimeshaenda kuzungumza nae mchana akaniambia niende na mtoto kesho amuone sasa nimekuja hapa kupata kwanza mawazo kutoka kwenu ndugu zangu.

Pia wife ameniambia ameshaangalia kwa watoto zaidi ya mmoja hapa kwenye ulimi pana tofauti kubwa sana na huyu mtoto wetu.pale Udowe huyu jamaa alihama nyumba ilivunjwa sasa ivi yupo K/koo na Chura.

Najaribu kuchambua shauri ninazopewa hapa nadhani mpaka kesho nitakuwa nimeshapata maamuzi sahihi.Asante sana!
 
We muuaji.kjaa
Huyu jamaa huwa anatafuta kutukanwa ili aanzishe ligi zisizokuwa na maana ila wengine tunachukulia ustaarabu tu tunamuacha kwani kurushiana maneno mabovu mitandaoni hatuwezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…